Nijuze Habari

14 Yanga kwenye alama nyekundu

Filed in Michezo by on 02/06/2022 0 Comments

14 Yanga kwenye alama nyekunduKLABU ya Young Africans SC huenda ikaachana na wachezaji wake 14 mwishoni mwa msimu huu wa 2021/2022, huku ikitarajia kujaza nafasi zao wakati wa usajili wa dirisha kubwa la usajili kuelekea msimu mpya wa NBC Premier League 2022/2023.

Nijuze Habari Application

14 Yanga kwenye alama nyekundu

14 Yanga kwenye alama nyekunduKLABU ya Young Africans SC huenda ikaachana na wachezaji wake 14 mwishoni mwa msimu huu wa 2021/2022, huku ikitarajia kujaza nafasi zao wakati wa usajili wa dirisha kubwa la usajili kuelekea msimu mpya wa NBC Premier League 2022/2023.

Wachezaji wanaotajwa kuwa kwenye mpango wa kuachwa klabuni hapo, ni wale ambao wameshindwa kufikia viwango vya benchi la ufundi la klabu hiyo chini ya Kocha Mkuu Mohamed Nabi mwenye umri wa miaka 57 raia wa Tunisia.

Miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa kwenye mpango wa kuachwa na Klabu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Jangwani ni David Bryson, Abdallah Shaibu, Deus Kaseke na Heritier Makambo.

Wengine ni Yusuph Athuman, Yassin Mustapha, Paul Godfrey, Crispin Ngushi, Dennis Nkane, Balama Mapinduzi, Chico Ushindi na Ibrahim Abdallah.

Wengine ni Walinda Lango Erick Johora na Ramadhan Kabwili, ambao hawajacheza hata mchezo mmoja wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) msimu huu wa 2021/2022.

Aidha klabu hiyo tayari imetangaza kuachana na aliyekuwa kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza, baada ya kumaliza mkataba wake, huku akihusishwa na utovu wa nidhamu wakati timu ilipoweka Kambi jijini Mwanza kwa maandalizi ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara โ€˜ASFCโ€.

UNAWEZA PIA KUSOMA๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.