Nijuze Habari

214 Wafutiwa Matokeo

Filed in Habari by on 15/01/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

BARAZA la Taifa la Mitihani (NECTA) limefuta Matokeo ya watahiniwa 214 katika Mitihani ya Darasa la Nne, Kidato cha Pili na Kidato cha Nne kwa hutuma za kufanya Udanganyifu.

Hayo yamebainishwa leo Jumamosi January 15, 2022 na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde wakati akitangaza Matokeo ya Darasa la Nne, Kidato cha Pili na Kidato cha Nne.

Dk Msonde amesema kati ya watahiniwa waliobainika kufanya udanganyifu, watahiniwa 83 ni wa darasa la Nne, watahiniwa 27 ni kidato cha Pili, wengine 102 ni Kidato cha Nne na wawili ni wa Mtihani wa maarifa (QT).

“Baraza la Mitihani limefuta Matokeo yote ya watahiniwa 214 waliofanya udanganyifu katika mtihani kwa mujibu wa kifungu cha 5(2) (i) na (j) Cha sheria ya Baraza la Mitihani sura ya 107 kikisomwa pamoja na cha 30(2)(b) cha kanuni za mitihani.

Dk Msonde amesema Baraza la Mitihani limezuia kutoa Matokeo ya watahiniwa 555 ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo.

“Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya mtihani kwa masomo ambayo hawakufanya kwa sababu ya ugonjwa mwaka 2021 kwa mujibu wa kifungu cha 32(1) cha kanuni za mitihani,” amesema Dk Msonde.

➡️ MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2021

➡️MATOKEO HA MTIHANI WA MAARIFA 2021

➡️MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE 2021

➡️MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI 2021

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.