Nijuze Habari App

Afunga ndoa na wanawake watatu siku moja

Filed in Habari by on 11/07/2023 0 Comments
Share This
 

SHINDA 50,000 BURE KILA SIKU BONYEZA HAPA


AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Afunga ndoa na wanawake watatu siku moja

Afunga ndoa na wanawake watatu siku moja, Mwanamume mmoja aitwaye Athumani Yengayenga mwenye umri wa miaka 35, mkazi wa Shanwe Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amewashangaza watu wengi kwa kuamua kufunga ndoa na wanawake watatu kwa siku moja huku akidai lengo lake lilikua ni kufunga ndoa na wanawake wanne kwa siku hiyo.

Hali hiyo imeibua maswali na mshangao kwa wakazi wa Mpanda na jamii kwa ujumla ambapo baadhi ya watu wamesema tukio hilo nila kwanza kutokea kwa Katavi na Tanzania kwa ujumla.

Akizungumzia ndoa yake Bwana harusi huyo amesema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na maumivu aliyoyapata mwanzo ya kuachwa na mke mmoja Aliyekua amemuoa.

Amesema baada ya kuachwa na mke wake huyo aliona kuna umuhimu wa kuoa wanawake wanne ili ikitokea ameachwa na mmoja atabakia na wake watatu ndipo alipoanza kazi ya kuwatafuta wanawake hao kwa nyakati tofauti.

Amesema kuwa alitumia saa nne kukaa kikao na wanawake hao ili kuwashawishi wakubaliane na wazo lake la kufunga ndoa na wote watatu kwa siku moja hivyo kufikia Julai 8,2023 alifanikiwa kufunga ndoa hiyo katika msikiti mkubwa wa ijumaa uliopo mjini Mpanda.

Wanawake hao wamesema kuwa wamefurahi kuolewa na wanaona jambo la kawaida japo mwanzo ilikua ni jambo gumu kulipokea hasa kwa mke mkubwa alipofikishiwa suala hilo na mume wake.

Mashaka Kakulukulu ni Shekh wa Mkoa wa Katavi amekili kufungisha ndoa hiyo huku akidai imefuata taratibu zote za dini na ametofautisha muda katika kufungisha ndoa hiyo.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

 

MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.

 
 

Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.

 

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *