telegram Nijuze Habari

ALLY Kamwe, Priva watua Yanga

Filed in Makala, Usajili by on 27/09/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

ALLY Kamwe, Priva watua Yanga

BAADA ya mchakato wa kufanyia Maboresho Idara ya Habari na Mawasiliano, Leo Jumanne September 27 2022, Klabu ya Yanga SC imetangaza kuongeza Majina kadhaa ambayo yataanza kazi rasmi katika idara hiyo.

Klabu hiyo imemteua Ally Kamwe kuwa Afisa Habari wa Klabu yetu akichukua nafasi ya Hassan Bumbuli ambaye mkataba wake na Yanga ulitamatika hivi Karibuni.

ALLY Kamwe, Priva watua Yanga

Ally Kamwe Afisa Habari Yanga SC

Ally Kamwe ni miongoni mwa vijana ambao wameleta Mabadiliko Makubwa sana katika tasnia ya Habari hususani uchambuzi kwa miaka ya hivi karibuni.

Ni miongoni mwa vijana wachache sana ambao wana weledi mkubwa na amekuwa na ushawishi wa kipekee kupitia mitandao ya kijamii kama Instagram.

Ubunifu wake wa mambo 10 umekuwa chachu kubwa ya kukua kwa kasi kwa jina lake na kumfanya kuwa miongoni mwa wachambuzi wenye ushawishi mkubwa.

Kamwe ana Elimu na uzoefu mkubwa kwani amefanya kazi katika vyombo mbalimbali hapa nchini na hivi sasa anajiunga Yanga akitokea Azam TV.

ALLY Kamwe, Priva watua Yanga

Privaldinho Digital Manager Yanga SC

Pia Yanga imemteua Priva Abiud maarufu kama (Privaldinho) kuwa Msimamizi Mkuu wa Digital (Digital Manager) kwa lengo la kusimamia platform zote za habari za Yanga.

Privaldinho alijizolea umaarufu kwenye mitandao ya kijamii kupitia upashaji wake wa habari hususani habari za usajili.

Priva ana Degree ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dodoma na hivi sasa anamalizia Masters ya Mass communication.

Amepitia vyombo mbalimbali vya habari kama vile Channel Ten na sasa anajiunga na Yanga SC akitokea Clouds Media Group.

ALLY Kamwe, Priva watua Yanga

Haji Mfikirwa Yanga

Aidha Yanga imemteua Haji Mfikirwa kuwa Mkurugenzi wa Wanachama, Mashabiki na Mahusiano ya Wanachama na Mashabiki (Fans And Members Engagement).

CPA Mfikirwa ni Msomi mwenye shahada ya Biashara na Mbobezi wa fani ya Uhasibu na alijiunga na Yanga SC mwaka 2020 na amefanikisha Maboresho Makubwa katika idara ya Fedha na utawala wa Klabu hiyo.

Kutokana na Utendaji wake mzuri na Mafanikio aliyoyapata katika Idara ya Fedha, Uongozi wa juu wa Klabu hiyo umeamua kumhamishia kwenye idara hii mpya ambayo ni mhimili Mkubwa katika muundo huo mpya wa uendeshaji wa Klabu.

Pamoja na hiyo Yanga pia inatarajia kutangaza nafasi kadhaa mchakato wa upatikanaji ukikamilika kwa nafasi zifuatazo

👉Mkurugenzi wa fedha na utawala
👉Meneja wa mmMiradi ( project manager )
👉Afisa uajiri

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *