Nijuze Habari

ARAFATI Makamu wa Rais mpya wa Yanga SC

Filed in Michezo by on 09/07/2022 0 Comments

ARAFATI Haji Yanga SCMwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi Yanga SC Malangwe Mchungahela ametangaza Arafat Ally Haji kuwa ndio mshindi wa nafasi ya Makamu wa Rais mpya wa Yanga SC.

Nijuze Habari Application

ARAFATI Makamu wa Rais mpya wa Yanga SC

ARAFATI Haji Yanga SCMwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi Yanga SC Malangwe Mchungahela ametangaza Arafat Ally Haji kuwa ndio mshindi wa nafasi ya Makamu wa Rais mpya wa Yanga SC.

Arafat amemshinda mpinzani wake Suma Mwaitenda kwa kupata kura 545 dhidi ya 234 za Mwaitenda, waliopiga kura walikuwa 785 na kura zilizoharibika zilikuwa ni sita (6) tu.

Wakati wa kugombea nafasi hiyo Arafat Ally Haji alitoa Vipaumbele vyake na kusema kuwa;

Matawi yetu ndio Afya ya klabu yetu, hakuna Yanga bila Matawi ya Klabu, tutashirikiana bega kwa bega na Matawi katika kuijenga Klabu yetu kwenye nyanja zote.

Pia tutaiongezea nguvu timu ya Wanawake pamoja na timu za Vijana tutaziboresha na kuziimarisha”

Sasa ni rasmi Rais wa Yanga SC ni Injinia Hersi Said na Makamu wake ni Arafat Haji.

Washindi wa Kamati ya Ujumbe Young Africans SCWashindi wa Kamati ya Ujumbe Young Africans SC.
1:Yanga Makaga
2:Seif Khamis Gulamali
3:Rogers Gumbo
4:Munir Seleman
5:Alexander Ngai

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.