Nijuze Habari

AZAM Pesa ni nini

Filed in Habari by on 13/06/2022 0 Comments

AZAM Pesa ni nini

Nijuze Habari Application

AZAM Pesa ni nini?

AZAM Pesa ni nini

AZAM Pesa ni nini? Azam Pesa ni huduma mpya ya kifedha nchini Tanzania.

Kampuni kubwa na iliyoenea katika nchi ya Tanzania pamoja na nchi jirani ‘Bakhresa Group’ imeleta sokoni huduma mpya ya kifedha ijulikanayo kama ‘Azam Pesa’.

Huduma hii ni kama zilivyo huduma nyinginezo za M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa, Halopesa and the like.

Ili kuielewa zaidi huduma hii, nitaenda katika mtindo wa Maswali na kisha majibu.

Je, Azam wameanzisha mtandao wao wa simu?
Hapana. Azam bado hawajaanzisha mtandao wao kama zilivyo kampuni kadhaa za mawasiliano hapa nchini.

Bali AzamPesa wameingia makubaliano na baadhi ya mitandao kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa huduma kupitia line za mitandao hiyo.

Mpaka sasa AzamPesa wameshakubaliana na Tigo, Airtel na Zantel. Hivyo huduma hii inapatikana katika line za mitandao tajwa.

Vodacom, Halotel na mitandao mingine bado wapo kwenye mazungumzo. Watakapokubaliana basi huduma hii itawezeshwa katika line hizo.

Je, huduma hi inahusika
na nini?
Kama ilivyo huduma zingine, huduma hii inahusika na;
1.Kutuma Pesa
2.Kutoa Pesa
3.Kulipia bili
4.Kulipia bidhaa za Azam

Je, huduma hii imeanza kufanya kazi?
Ndiyo, huduma hii imeshaanza kufanya kazi kwa wateja wote waliosajiliwa.

Je, najiungaje na huduma hii?
Fika katika duka la wakala na uweze kusajiliwa. Kinachohitajika ni namba yako ya simu pamoja na namba yako ya NIDA. Ndani ya dakika mbili tayari utakuwa umeshasajiliwa kuwa mteja wa AzamPesa.

Je, huduma naweza kupata vifurushi ‘bundles’ maalum vya Azam?
Hapana. Kama ambavyo nilijwishaeleza hapo juu kwamba Azam bado hawajaanzisha mtandao wao hivyo swala la vifurushi linabakia kuwa maamuzi ya mtandao husika.

Je, huduma hii naipata wapi?
Huduma hii inapatikana katika mikoa yote Tanzania. Ijapokuwa bado haijatapakaa kila mahali lakini upatikanaji wake katika maeneo mengi ya miji ni uhakika.

Je, menu ‘ussd’ ya AzamPesa ni ngapi?
Baada ya kusajiliwa, utabadili namba ya siri. Hivyo utabonyeza *150*08# na kuweza kupata huduma ya AzamPesa.

Kama una swali lolote kuhusiana na huduma za AzamPesa, basi karibu.

UNAWEZA PIA KUSOMA👇👇👇

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.