Nijuze Habari

AZAM yasajili wanne faster, watatu kutoka nje, yupo Ndalla wa Plateau United

Filed in Usajili by on 02/07/2022 0 Comments

Tape Edinho Azam FCKLABU ya Azam FC imekamilisha Usajili wa kiungo mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Tape Edinho, kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka ES Bafing ya kwao Ivory Coast, ambapo mkataba huo utamfanya kuhudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2025.

Nijuze Habari Application

AZAM yasajili wanne faster, watatu kutoka nje, yupo Ndalla wa Plateau United

Tape Edinho Azam FCKLABU ya Azam FC imekamilisha Usajili wa kiungo mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Tape Edinho, kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka ES Bafing ya kwao Ivory Coast, ambapo mkataba huo utamfanya kuhudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2025.

Tape Edinho Azam FCNyota huyo mwenye uwezo mkubwa, amesaini mkataba huo mbele ya mmiliki wa timu hiyo, Yusuf Bakhresa na Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’.

Kipre Junior Azam FCKlabu hiyo pia imekamilisha Usajili wa kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast pia, Kipre Junior kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka Sol FC ya kwao Ivory Coast, akisaini mkataba huo mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin.

Kipre Junior Azam FCKiungo huyo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 22, aliwahi kuwatumikia vigogo wa Ivory Coast, ASEC Mimosas miaka ya 2018-2020.

Isah Ndala Azam FCAzam FC pia imefanikiwa kuinasa saini ya kiungo mkabaji kutoka Nigeria, Isah Ndala kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Plateau ya Nigeria, akisaini mkataba huo mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa na Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin.Isah Ndala Azam FC

Kiungo huyo, mwenye umbo kubwa, sifa ya ukabaji na kupiga pasi, anakuja kuimarisha eneo la kiungo, ambapo Septemba mwaka huu atakuwa anatimiza umri wa miaka 20.

Isah Ndala Azam FCAidha mbali na kucheza Plateau, Ndalla amepita pia katika timu ya Sevan ya Armenia na Nasarawa United ya Nigeria.

Cleophace Mkandala Azam FCKlabu ya Azam FC imekamilisha Usajili wa kiungo Mshambuliaji, Cleophace Mkandala, kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Dodoma Jiji FC.Cleophace Mkandala Azam FC

Kiungo huyo aliyefanya vizuri msimu uliopita, amesaini mkataba mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’.

Mkandala mwenye umri wa miaka 21 ni mmoja wachezaji vijana wanaochipukia vizuri, amesaini mkataba huo wenye kipengele cha kuongeza ndani ya miezi sita na hiyo itatokana na kiwango atakachokionyesha.

Cleophace Mkandala Azam FCAidha mbali na kuicheza Dodoma Jiji, Mkandala pia amewahi kucheza kwa misimu mitatu ndani ya kikosi cha maafande wa Tanzania Prisons, 2018-2019 hadi 2020-2021.

Huo unakuwa usajili wa kwanza wa Azam FC kwa wachezaji wa ndani kuelekea msimu ujao 2022/2023, ikiwa tayari imetangaza kusajili wachezaji watatu wa kigeni, viungo washambuliaji, Kipre Junior na Tape Edinho, wanaotokea Ivory Coast pamoja na kiungo mkabaji kutoka Nigeria, Isah Ndala.

Dani Cadena Kocha wa Makipa Azam FCAzam FC pia imemtambulisha, Dani Cadena, kocha wa zamani wa makipa wa klabu za Ligi Kuu Hispania (La Liga) Sevilla na Real Betis kama kocha mpya wa magolikipa kwenye Klabu hiyo.Dani Cadena Kocha wa Makipa Azam FC

Kocha huyo ambaye pia ameshafanya kazi nchini China na Asaudi Arabia, ana uzoefu mkubwa na elimu ya juu ya Shirikisho la Soka la Ulaya UEFA.

We are delighted to welcome Mr. Dani Cadena (Former Goalkeeping Coach from Sevilla and Real Betis) to Azam FC.Dani Cadena Kocha wa Makipa Azam FC

A highly motivated and experienced Goalkeeping Coach with the highest European Degree(UEFA).

“If you are going to have a dream, dream Big”.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.