Nijuze Habari

BINGWA Ligi Kuu kuondoka na Sh600 milioni, Kombe jipya latambulishwa

Filed in Michezo by on 09/06/2022 0 Comments

BINGWA Ligi Kuu kuondoka na Sh600 milioni, Kombe jipya latambulishwaMTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Almas Kasongo ametambulisha Kombe Jipya atakalopewa Bingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu wa 2021/2022.

Nijuze Habari Application

BINGWA Ligi Kuu kuondoka na Sh600 milioni, Kombe jipya latambulishwa

BINGWA Ligi Kuu kuondoka na Sh600 milioni, Kombe jipya latambulishwaMTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Almas Kasongo ametambulisha Kombe Jipya atakalopewa Bingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu wa 2021/2022.

Akiongea wakati wa Uzinduzi huo Kasongo amewashukuru wanahabari na wadau wote wa mpira kwa michango yao katika kukuza soka la nchi hii, lakini pia namna ambavyo wanauongelea mpira wa nchi pamoja na changamoto walizonazo Bodi ya Ligi ambazo yeye kama Mtendaji Mkuu anaridhika nazo na anazifanyia kazi kutoka changamoto kuwa Fursa.

Kasongo pia ameongeza kuwa Bodi ya Ligi kwa kushirikiana na TFF imejipanga kufanya mambo kisasa kwani ina mpango wa kuandaa Replica au mfanano wa Kombe halisi la Mshindi wa Ligi Kuu ya NBC ili pale inapotokea hatua kuwa hadi siku ya mwisho Bingwa anakuwa hajafahamika basi Replica hizo zinasambaa katika Viwanja husika ambavyo ikitokea Bingwa akapatikana basi anakabidhiwa Kombe lake mara moja.

Aidha Kasongo amewashukuru na kuwapongeza wadhamini mbalimbali wa soka nchini wakiwemo NBC, Azam Media na wengineo kwa mchango wake katika kuiheshimisha Ligi Kuu nchini kwani hadi sasa Ligi Kuu ikiwa katika raundi ya 24 haijulikani timu gani imeshuka daraja, timu gani imejihakikishia kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu nchini.

UNAWEZA PIA KUSOMA👇👇👇

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.