Nijuze Habari

CAF Super Cup yazinduliwa, Bingwa kuvuna Mabilioni

Filed in Michezo by on 10/08/2022 0 Comments

CAF Super Cup yazinduliwa, Bingwa kuvuna MabilioniKUPITIA Mkutano wake Mkuu wa Kawaida wa 44, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limezindua Mashindano mapya ya Africa Super League yatakayoshirikisha Vilabu 24.

Nijuze Habari Application

CAF Super Cup yazinduliwa, Bingwa kuvuna Mabilioni

CAF Super Cup yazinduliwa, Bingwa kuvuna MabilioniKUPITIA Mkutano wake Mkuu wa Kawaida wa 44, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limezindua Mashindano mapya ya Africa Super League yatakayoshirikisha Vilabu 24.

Vilabu hivyo vitatoka katika kanda tatu za kisoka Afrika huku kila ukanda ukitoa vilabu vinane (8) vitakavyounda Ligi hiyo itakayohusisha Mataifa 16 Barani Afrika.

CAF imetaja sababu Kuu ya kuanzisha Mashindano hayo kuwa ni kukuza thamani ya mpira wa Miguu Afrika kupitia uwekezaji, udhamini pamoja na mifuko ya maendeleo.

Africa Super League imetajwa kuwa itachezwa kwa kipindi cha miezi 10 kuanzia August hadi May kila mwaka na itakuwa na jumla ya michezo 197.

Fainali za mashindano hayo ambayo imepewa jina la SuperFinal itachezwa mwishoni mwa mwezi May katika Uwanja utakaoandaliwa kuwa na mfano wa Fainali za SuperBowl (Marekani).

CAF Super Cup yazinduliwaKatika mkutano huo, Rais wa CAF, Dkt. Patrick Motsepe amesema ndani ya miezi kadhaa ijayo, watatangaza mfumo mzima wa mashindano hayo na tarehe ambayo mashindano hayo yatatarajiwa kuanza.

Patrice Motsepe pia amesema kuwa Michuano ya Super Cup inayotarajiwa itazinufaisha Klabu zote zitakazoshiriki.

Akizungumza katika Mkutano wa mwaka wa CAF unaofanyika jijini Arusha, Motsepe amesema wanafahamu changamoto kubwa inayokwamisha maendeleo ya soka la Afrika ni fedha pamoja Changamoto ya Viwanja.

Amesema kupitia mashindano ya CAF Super Cup klabu zitapata fedha nyingi

Ukiacha viwanja tatizo kubwa kwa mpira wa Afrika ni fedha. Nimshukuru Rais wa FIFA Gianni Infantino kwa kutupatia wazo hili”

“Kupitia mashindano haya mapya ya CAF SUPER LEAGUE klabu zitapata fedha nyingi ambapo kwanza kila Klabu itapata dola milioni 2.5 kwaajili ya kusajili Wachezaji na Gharama za Michuano kama Usafiri na Hotel lakini pia Bingwa atapata dola Milioni 100.CAF Super Cup

Vilabu 24 Vinavyotarajwa kuwa vinaweza Kushiriki CAF Super League

1:Al Ahly 🇪🇬
2:Zamalek🇪🇬
3:Pyramid 🇪🇬
4:Al Masry🇪🇬
5:Wydad AC 🇲🇦
6:Raja Athletic 🇲🇦
7:RS Berkane 🇲🇦
8:Esperance 🇹🇳
9:Etoil Sportive Du Suhel 🇹🇳
10:Orlando Pirates 🇿🇦
11:Kaizer Chiefs 🇿🇦
12:Mamelodi Sundowns 🇿🇦
13:JS Kabyile🇩🇿
14:CR Belouzidad 🇩🇿
15:E.S Setif 🇩🇿
16:TP Mazembe 🇨🇩
17:Horoya AC 🇬🇳
18:SC Enyimba🇳🇬
19:Petro de Luanda 🇦🇴
20:Simba SC 🇹🇿
21:Asante Kotoko🇬🇭
22:Al Hilal 🇸🇩
23:Asec Mimosas🇨🇮
24:Coton Sport🇨🇲CAF Super Cup yazinduliwa

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.