Clatous Chama akutana na Rungu la TFF

Filed in New by on 21/05/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

Clatous Chama akutana na Rungu la TFF

Clatous Chama akutana na Rungu la TFFKAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Mei 19, 2023 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;

Ligi Kuu ya NBC

  • Mechi Namba 222: Simba SC 3-0 Ruvu Shooting FC

Mchezaji wa klabu ya Simba, Clatous Chama amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa klabu ya Ruvu Shooting, Abal Kassim Suleiman tukio ambalo lilitokea wakati wachezaji hao hawagombei mpira, jambo lililosababisha mwamuzi wa mchezo ashindwe kuona.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 41:5(5.2) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.

First League

  • Mechi Namba FLT8-03: African Lyon 1-2 Rhino Rangers FC

Kiongozi wa klabu ya African Lyon ya mkoani Dar es Salaam, Salehe Hassan maarufu kama Mkele amefungiwa miezi sita (6) na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kumtolea lugha za kejeli na matusi Kamishna wa mchezo tajwa hapo juu ambaye alimwelekeza atoke nje ya chumba cha kuvalia wakati wa ukaguzi wa timu.

Kamishna wa mchezo wa hatua ya Nane Bora alifanya maamuzi hayo baada ya kuona kiongozi huyo wa African Lyon anafanya vurugu zilizoathiri zoezi la kikanuni la ukaguzi wa timu kwenye uwanja wa Azam Complex Aprili 25, 2023.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 47:3 ya First League kuhusu Udhibiti kwa Viongozi.

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi inqzikumbusha klabu zote za Ligi Kuu ya NBC, Ligi ya Championship na First League kuhakikisha Viongozi na Wachezaji wake wanaendelea kufuata na kutekeleza masharti yote ya Kanuni za Ligi katika kipindi hiki cha michezo ya mtoano (play-offs) na michezo ya ukingoni mwa msimu wa 2022/2023 wa Ligi Kuu ya NBC.

Kamati inaamini huu ni wakati wa klabu kujikita katika maandalizi ya timu kiufundi kuelekea michezo hiyo na kujiepusha na masuala mengine yote yasiyo ya kiuanamichezo na yanayoweza kuchafua taswira ya Ligi zetu na mpira wetu kwa ujumla.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *