Dalili za Saratani ya Tezi Dume

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


Dalili za Saratani ya Tezi Dume

Dalili za Saratani ya Tezi Dume
SARATANI YA TEZI DUME
Moja ya maradhi yanayoshuhudia kampeni kubwa kukabiliana nayo katika miaka ya hivi karibuni duniani ni pamoja na saratani ya tezi dume kutokana na ukubwa wa athari inazosababisha.
Ni maradhi yanayoshika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na saratani kwa wanaume duniani.
Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea.Hata hivyo, satarani ya tezi dume kwa sasa inawapata zaidi wanaume kuanzia miaka 25.
Maana ya saratani
Saratani maana yake ni ukuaji holela bila mpangilio wa seli baada ya kuparanganyika kwa mfumo wa seli unaodhibiti ukuaji na uhai wake. Na uvimbe wa kawaida wa tezi maana yake ni kuwa seli zimetutumka tu lakini hakuna mparanganyiko wa seli wala kukua kwa kusambaa kiholela kama ilivyo kwa saratani.
Hivyo, ndio maana kuna tatizo la kuvimba tezi dume na wengine kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume wenye umri mkubwa.
Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu.
Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).
Kazi ya tezi dume
Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la kujamiana. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hutengeneza shahawa (semen).
Majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya uzazi, tayari kwa utungisho na yai la kike.
Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo isiporekebishwa, huua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu..
Vyanzo Vinavyopelekea Tezi Dume Kutanuka:
Tatizo la kutanuka kwa tezi dume limekuwa kwa kasi sana hii ni kutokana na mitindo ya maisha wanaume wengi wanayoishi. Pia na elimu ndogo iliyoko kwenye jamii kuhusu afya zao.
Vifuatavyo ni vyanzo vya kutanuka kwa tezi dume:
– Ukosefu wa lishe kamili na Virutubisho muhimu mwilini.
– Uwepo wa sumu nyingi mwilini.
– Kutokufanya mazoezi.
– Matumizi ya pombe kali, na uvutaji wa sigara.
– Uzito mkubwa (uliopindukia, uliokithiri), na Kitambi.
– Kutokukaa sawa kwa vichocheo vya mwili (Hormone Imbalance).
– Msongo wa mawazo (Stress).
– Magonjwa ya zinaa.
– Umri mkubwa.
– Upasuaji wa korodani, kuzaliwa na korodani moja.
– Historia ya Familia (Kurithi).
– Mazingira (Ethnicity).
Dalili za Saratani ya Tezi Dume
- Udhaifu katika utoaji wa mkojo, mkojo hauishi.
- Kwenda kukojoa mara kwa mara.
- Damu ndani ya mkojo.
- Kushindwa kukojoa.
- Maumivu ya kiuno na mifupa ya nyonga.
- Wagonjwa wengi huanza maumivu ya nyonga kama ni dalili za awali.
- Udhaifu katika utoaji wa mkojo pia kunaweza kutokea kwa kuvimba kwa tezi dume bila ya saratani.
- Damu kwenye mkojo nakushindwa kumaliza mkojo ni ishara tosha ya kuwa tezi dume imeathirika.
Dalili za mtu aliyeathirika
- Maumivu ya mifupa hasa chini ya mgongo, kiuno na mbavu
- Miguu kuwa dhaifu
- Kushindwa kumudu tendo la ndoa, au Kuhisi maumivu makali wakati unamaliza tendo la ndoa
- Kushindwa kuzuia mkojo, pindi unapohisi kukojoa
- Kushindwa kuzuia haja kubwa (kinyesi cha maji maji)
- Tumbo kuja gesi mara kwa mara
UCHUNGUZI
Wanaume wote wanapaswa kufanya uchunguzi wa saratani ya tezi dume kuanzia miaka 50. Kwa wale wenye historia katika familia wanapaswa kuanza wakiwa na umri wa miaka 45.
Uchunguzi unafanyika kwa njia zifuatazo
- Uchunguzi kwa cancer marker kwa kuchunguza damu (PSA).
- Uchunguzi kwa njia ya kipimo cha njia ya haja kubwa (DRE)
- Biopsy.
- Ultrasound.
- X-ray.
- Bone scan.
Jinsi ya kutibu saratani ya tezi dume
- Upasuaji.
- Mionzi
- Dawa ya saratani
- Homoni.
Matibabu hutegemea
- Ngazi na ukali wa ugonjwa.
- Je, ugonjwa upo ndani ya tezi dume tu au umesambaa.
- Umri na afya ya mgonjwa.
- Magonjwa ambatanishi na saratani hiyo, shinikizo la damu, matatizo ya moyo na kisukari.
TIBA
UPASUAJI
- Kuondoa tezi dume yote peke yake inaweza ikatosha.
- Kuondoa tezi dume na tezi jirani.
- Kuondoa tezi dume na kuhasi
- Kuondoa tezi dume kidogo kupitia njia ya mkojo na kumpa mgonjwa tiba shufa.
MIONZI.
- Sawa na upasuaji inaweza kuondoa ugonjwa iwapo haujasambaa.
- Mionzi pia hutolewa kama tiba shufaa.
DAWA YA SARATANI
Baadhi ya wagonjwa hufaidika na tiba hii, dawa hutolewa kwa muda mfupi na kufuatilia maendeleo ya mgonjwa kwa kufanya PSA,dawa inaweza kuwa moja au mchanganyiko.
HOMONI
Hutolewa mfullulizo kwa njia ya vidonge au sindano.
Ufuatiliaji wa karibu
Ni muhimu kufuatilia hali ya tezi isirejee baada ya ugonjwa kutibiwa kwa kufanya kipimo cha PSA mara kwa mara angalau miezi mitatu mara moja.
Madhara ya Tezi Dume Iliyotanuka:
- Kibofu cha mkojo kuuma: hivyo hupelekea mkojo kurudi juu, na kuharibu figo na Ini … … n.k.
- Kufunga kwa njia ya mkojo kabisa
- Figo kushindwa kufanya kazi (Kidney Failure)
- Kushindwa kumudu tendo la ndoa (Ndoa zinavunjika)
- Ugumba (Infertility, Frigidity for men)
- Kutokea kwa majipu sehemu ya Tezi Dume
- Kifo
Athari zitokanazo na matibabu mbalimbali yaliyotajwa.
Upasuaji
Unaweza kusababisha kutoweza:
- Kuzuia mkojo
- Kupoteza nguvu za kiume.
Homoni
- Homoni huongeza joto mwilini
- Kupungukiwa na nguvu za kiume
- MSIMAMO Kundi D CAF Confederation Cup 2022-2023
- MSIMAMO Kundi C CAF Champions League 2022-2023
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: Dalili za Saratani ya Tezi Dume, Dalili za tezi dume na tiba yake, Madhara ya upasuaji wa tezi dume, Picha ya tezi dume, Sababu ya kupata tezi dume, Tezi dume na nguvu za kiume, Tezi dume ni nini, Tiba asili ya tezi dume, Vyakula vinavyozuia tezi dume