EWURA bei mpya za Mafuta Tanzania August 2022
JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA
JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA
AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
EWURA bei mpya za Mafuta Tanzania August 2022
BEI ya mafuta nchini Tanzania, imepanda tena mwezi huu August na kuivuka ile ya July 2022 ambapo petroli imepanda kwa Sh190 kwa kila lita na Sh179 kwa kila lita ya dizeli huku mafuta ya taa yakipanda kwa Sh323 kwa kila lita kwa Jiji la Dar es Salaam.
Katika taarifa iliyotolewa Jumanne Agosti 02, 2022 na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), bei ya rejareja Jijini Dar es Salaam itakuwa Sh 3,410 kwa lita moja ya petroli na Sh3,322 kwa dizeli huku mafuta ya taa yakifika Sh3,765.

Kutokana na bei hiyo mpya ambayo itaanza kutumika kesho, petroli imepanda kwa Sh190 kwa kila lita ambapo mwezi uliopita iliuzwa Sh3,220 na Sh179 kwa kila lita ya dizeli ambayo mwezi uliopita iliuzwa Sh3,143 huku mafuta ya taa yakipanda kwa Sh323 kwa kila lita ambako mwezi uliopita yaliuzwa Sh3,442.
Ewura imesema bei hizo mpya ambazo zitaanza kutumika Leo Jumatano Agosti 03, 2022 zimejumuisha ruzuku ya Sh100 bilioni iliyotolewa na Serikali vinginevyo, lita ya petroli ngeuzwa Sh3,630 na dizeli Sh3,734 jijini Dar es Salaam.
MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.
Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.
“Bei za Mafuta katika soko la dunia zimeendelea kuongezeka na kusababisha bei za mafuta katika soko la ndani kuongezeka pia.”
“Ili kupunguza madhara ya ongezeko hilo katika soko la ndani, Serikali imetoa ruzuku ya bilioni 100 kwaajili ya bei za mafuta hapa nchini kwa August 2022. Serikali kwa kutoa ruzuku hiyo, imepunguza bei za bidhaa za mafuta kwa Agosti 2022,” imeeleza taarifa
TAZAMA HAPA CHINI BEI MPYA ZA MAFUTA KWA TANZANIA NZIMA.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
