Nijuze Habari App

Fahamu Utaratibu wa Kuomba Leseni ya Biashara ya Kituo cha Mafuta

Filed in Makala by on 10/04/2023 0 Comments
Share This

JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA


JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA


AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Fahamu Utaratibu wa Kuomba Leseni ya Biashara ya Kituo cha Mafuta

Fahamu Utaratibu wa Kuomba Leseni ya Biashara ya Kituo cha Mafuta, Mafuta tanzania,Kazi ya kuuza mafuta sheli,Jinsi ya kufanya kazi sheli,Mtaji wa kujenga sheli,Ramani za sheli.

Fahamu Utaratibu wa Kuomba Leseni ya Biashara ya Kituo cha Mafuta

Maombi ya leseni yanapitia mfumo wa kielektroniki Licensing and Order Information System (LOIS), unaopatikana kwenye tovuti ya EWURA www.ewura.go.tz.

Ambatisha maombi na nakala za nyaraka zifuatazo zilizothibitishwa na mwanasheria:
(a) Cheti cha Usajili wa Kampuni au Leseni ya Biashara;
(b) Hati ya kiwanja au uthibitisho kutoka Mamlaka husika iliyoruhusu ujenzi wa kituo eneo hilo.
(c) Kibali cha ujenzi kutoka Halmashauri au Manispaa husika.
(d) Cheti cha Tathmini ya Athari ya Mazingira kutoka Baraza la Hifadhi ya Mazingira.
(e) Cheti cha mlipa kodi (TIN Certificate).
(f) Cheti cha zimamoto kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.
(g) Kibali cha ujenzi kutoka EWURA.
(h) Orodha ya miundombinu iliyopo katika eneo hilo.

Kwa upande wa matanki onesha ujazo wake. (i) Mchoro wa kituo uliosainiwa na Mhandisi aliyesajiliwa na Bodi ya Wahandisi Tanzania ukionesha yafuatayo:
(i) umbali uliopo kati ya miundombinu ya kituo cha mafuta;
(ii) mahali pa kuingilia na kutokea kituoni;
(iii) mpaka wa kiwanja; na
(iv) eneo zitakapofungwa pampu.

Baada ya kukamilisha, mfumo wa LOIS utakuelekeza kulipa ada ya maombi ya leseni na kiasi cha ada hiyo.

Maombi yanatakiwa kukidhi vigezo vifuatayo:
(a) Hakuna mushkeli kwenye nyaraka zilizowasilishwa;
(b) Hakuna pingamizi ambalo halijafikiwa muafaka; na
(c) Ukaguzi umefanyika na ujenzi wa kituo umezingatia viwango vya Shirika la Viwango la Taifa (TBS) TZS 1115: 2009 na TZS 1079: 2008.

Mwombaji yeyote wa leseni ya rejareja ya mafuta, sharti afanye maombi kwa njia ya kieletroniki kupitia http://www.ewura.go.tz/lois.

Taarifa muhimu zinazohitajika kuambatanishwa katika maombi hayo ni:
(a) Nakala ya nyaraka za usajili wa Kampuni au Leseni ya Biashara;
(b) Nakala ya Hati Miliki ya kiwanja palipojengwa kituo cha mafuta au uthibitisho
kutoka Mamlaka husika iliyoruhusu ujenzi wa kituo hicho.
(c) Nakala ya kibali cha ujenzi kutoka Halmashauri au Manispaa husika.
(d) Nakala ya Cheti cha Tathmini ya Athari ya Mazingira (Environmental Impact Assessment Certificate) kinachotolewa na Baraza la Hifadhi ya Mazingira.
(e) Nakala ya cheti cha mlipa kodi (TIN Certificate).
(f) Nakala ya cheti cha zima moto (Fire Safety Certificate) kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.
(g) Kibali cha ujenzi kutoka EWURA (kwa vituo vilivyojengwa baada ya Aprili 2009).
(h) Orodha ya miundombinu iliyopo katika eneo hilo. Kwa upande wa matanki uooneshwe ujazo wake.

(i) Mchoro wa kituo ambao umesainiwa na Mhandisi aliyesajiliwa na Baraza la Wahandisi Tanzania ukionesha yafuatayo:
(i) umbali uliopo kati ya miundombinu ya kituo cha mafuta;
(ii) mahali pa kuingilia na kutokea kituoni;
(iii) mpaka wa kiwanja;
(iv) mahali pampu zinapotegemewa kufungwa; na
(j) Stakabadhi ya malipo ya ada ya maombi ya leseni.

MASHARTI YA KUPEWA LESENI YA REJAREJA YA KUENDESHA BIASHARA YA MAFUTA

Pamoja na kuwasilisha nyaraka zilizotajwa, kituo cha mafuta sharti kikaguliwe ili kuona kama kinakidhi masharti ya kupewa leseni. Masharti hayo ni pamoja na:

(a) Kuwa na vifaa vya kutosha vya kuzimia moto: Angalau ndoo moja ya mchanga na mtungi mmoja wa kilogramu 9 aina ya “ABE” kwa kila eneo ilipo pampu.
(b) Kuwepo switchi ya dharura iliyowekwa sehemu inayoonekana na kufikika kwa urahisi na mtu yeyote kwaajili ya kuzima umeme. Swichi iandikwe “SWICHI YA DHARURA”.
(c) Kuwepo na vyoo safi na vya kutosha kwa ajili ya wafanyakazi wa kituo na wateja kwa ujumla. Viwepo vyoo vya wanaume na wanawake.
(d) Alama za kutosha za usalama zinazoonekana vizuri na mteja anapoingia hapo kituoni. Alama hizo ni pamoja na: Zima Injini, Zima Simu na Usivute Sigara.
(e) Matanki, vifaa vya kupimia ujazo wa matanki (dip rods) na pampu lazima viwe vimehakikiwa na Wakala wa Vipimo (WMA). Aidha, pampu sharti ziwe katika hali nzuri ya kufanya kazi.
(f) Mifuniko ya sehemu ya kushushia mafuta na pampu sharti iandikwe ili kuonesha aina ya mafuta yaliyomo au yanayouzwa.
(g) Mifuniko ya matanki ya mafuta sharti ipakwe rangi zifuatazo: Petroli – Nyekundu, Dizeli – Njano na Mafuta ya taa – Bluu
(h) Kila mfuniko wa tanki na mahali pa kuteremshia mafuta vitengenezwe kulingana na viwango vinavyokubalika katika tasnia ya mafuta.
(i) Kituo kiwe kimesakafiwa kwa zege angalau mita nne (4) kuzunguka maeneo yote ya pampu na mahali pa kushushia mafuta na pia kiwe na mfereji uliojengwa vizuri na unaoungana na kitenganisha maji na mafuta (oil/water separator).
(j) Kitenganisha maji na mafuta sharti kiwe na vyumba (chemba) vitatu na kila chumba kiwe na urefu usiopungua mita 1, upana wa mita 2 na kimo cha mita 1. Pia, sharti kiwe na mfuniko unaoweza kufunguliwa kwa urahisi na kuwekwa vali ya kufunga na kufungua mahali pa kutolea maji safi.
(k) Kila tanki la mafuta liwe limeunganishwa na bomba la kupumulia (vent pipe) lenye kimo kisichopungua mita 3.5. Bomba hizo ziwe angalau mita 1.5 kutoka jengo lolote na angalau mita 4.5 kutoka chanzo chochote cha kuingiza hewa au kusababisha moto kama vile dirisha, kiyoyozi, jenereta n.k.
(l) Eneo la pampu liwe limejengewa vizuizi vya kukinga pampu zisigongwe na gari (crush barriers). Vizuizi hivyo viwe na kimo kisichopungua mita moja kutoka sakafu ya kituo.
(m) Kituo kiwe kimejengewa paa (canopy) linalokidhi viwango vinavyotakiwa katika ujenzi wa vituo vya mafuta. Kimo cha paa kisipungue mita 5 na upana wa mita 3 kila upande kutoka katikati ya pampu.
(n) Kituo kiwe katika hali ya usafi.
(o) Kuwepo kwa waya wa kuzuia mwako wa umeme (spark) ambao unaunganishwa na gari la mafuta wakati wa kuteremsha mafuta.

Kituo cha mafuta kinachokidhi masharti tajwa hapo juu, ndicho hupewa leseni na EWURA. Vituo vya mafuta ambavyo havikidhi masharti ya kupewa leseni, haviruhusiwi kufanya biashara hadi hapo vitakapokuwa vimekidhi masharti yote.

ADA NA MUDA WA UHAI WA LESENI

Ada ya leseni ni Shillingi milioni moja (1.000.000/=). Muda wa leseni ni miaka mitano (5). Baada ya uhai wa leseni, mwenye kituo anatakiwa aombe kuhuisha leseni kwa kujaza fomu ya maombi na kuipeleka EWURA.

UJENZI WA VITUO VYA GHARAMA NAFUU – VIJIJINI
1. Utangulizi

1.1 Mahitaji ya mafuta ya petroli na dizeli maeneo ya vijijini yanazidi kuongezeka. Ongezeko hili linatokana na kushamiri kwa shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na usafiri wa pikipiki maarufu kama “boda boda”.

1.2 Hata hivyo, maeneo mengi ya vijijini hayana vituo vya mafuta kutokana na ukweli kwamba, wawekezaji wa biashara hiyo wenye mitaji mikubwa husita kujenga vituo vya kuuzia mafuta Vijijini kwa kuona maeneo hayo hakuna biashara ya kutosha .

1.3 Matokeo yake, wafanyabiashara wenye mitaji midogo na wasio na uzoefu katika biashara ya mafuta, huingia kwenye biashara hii. Kutokana na mitaji yao midogo na kutokuwa na uzoefu, wafanyabiashara hawa huanza kufanya biashara ya mafuta kwa kutumia miundo mbinu hafifu na isiyo salama kama vile kuhifadhi mafuta kwenye mapipa, madumu ya plastiki na kuyauza kwa kutumia chupa za plastiki au njia nyingine isiyo salama.

 

MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.

 
 

Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.

 

1.4 Uhifadhi wa mafuta kwa namna hiyo ni hatari kwa Usalama, Afya na Mazingira. Ni dhahiri kuna matukio mengi ya moto ambayo yamesababishwa na uhifadhi wa mafuta majumbani au kwenye vibanda vya biashara. Ajali hizo za moto, zimegharimu maisha ya watu na kuharibu mali. Pia, wafanyabishara katika maeneo hayo wako hatarini kupata magonjwa ya kansa ya ngozi kutokana na kushika mafuta wakati wa kutoa huduma hiyo. Kwa upande mwingine, mafuta humwagika ardhini na kuharibu mazingira.

1.5 Kuhifadhi mafuta kutumia vyombo vya plastiki kunaharibu ubora wa mafuta hayo na hasa mafuta ya petroli. Mafuta na vyombo vya plastiki vina asili moja. Ubora wa mafuta ya petroli pia unaweza kuathiriwa na mwanga wa jua. Hivyo, vyombo vya moto vinavyo tumia mafuta yanayohifadhiwa kwenye vyombo vya plastiki viko hatarini kupata madhara kwa sababu ya kutumia mafuta ambayo hayana ubora unaohitajika.

1.6 Biashara ya mafuta ya petroli ni muhimu sana, lakini ni hatari ikiwa itafanyika kiholela bila kufuata misingi ya usalama na viwango. Hivyo ni vyema mafuta ya petroli yakahifadhiwa na kuuzwa kwenye miundombinu ambayo imetengenezwa kwa ajili ya kazi hiyo. Lengo ni kulinda usalama, afya, ubora wa mafuta na mazingira.

1.7 Moja ya miundombinu ambayo inatimiza lengo tajwa hapo juu ni vituo vya kuuzia mafuta. Sababu kubwa ni kuwa, kwenye kituo cha mafuta, matenki ya kuhifadhia mafuta yanafukiwa chini ya ardhi. Hivyo, hata moto ukitokea si rahisi mafuta yaliyo ndani ya matenki hayo kulipuka.

1.8 Kipeperushi hiki kimelenga kutoa maelezo kwa kifupi juu ya ujenzi wa vituo vya gharama nafuu kwa kuelezea vitu muhimu na vya msingi vinavyotakiwa kuzingatiwa wakati wa kujenga kituo cha mafuta. Vilevile, Kipeperushi hiki kinaelezea Kanuni za EWURA za ujenzi wa vituo vijijini ambazo zilitungwa mahsusi kwa ajili ya kupunguza gharama za uwekezaji wa vituo hivyo.

1.9 Ni lengo la EWURA kutengeneza mazingira ambapo watu wa Vijijini wanakuwa na haki sawa na watu wa Mijini katika upatikanaji wa bidhaa ya mafuta kwa hali ya ubora na usalama unaohitajika na kwa bei nafuu.

1.10 Ni matumaini ya EWURA kwamba, Kipeperushi hiki kitatoa mwanga kwa wawekezaji na wafanyabiashara wa mafuta ya petroli nchini namna ambavyo uwekezaji wa vituo vya mafuta Vijijini unavyoweza kufanywa kwa gharama nafuu na kuwawezesha watumiaji wa mafuta hayo kupata huduma nzuri zaidi na salama bila kumuathiri mfanyabiashara wa mafuta.

2 Mahitaji na Mambo ya Kuzingatia Wakati wa Ujenzi

Ili uweze kujenga kituo unatakiwa kuzingatia yafutatayo:

(a) Uwe na kiwanja ambacho Mamlaka husika (mfano: Halmashauri ya kijiji) imeridhia kitumike kwa ajili ya biashara ya kituo cha mafuta. Ili kukidhi viwango vya usalama (safety distance requirements), kiwanja kinachofaa kujenga kituo cha mafuta kinatakiwa angalau kiwe na ukubwa wa mita za mraba 400.

(b) Uwe angalau na tenki moja (1) la kuhifadhia mafuta. Kama utauza aina zaidi ya moja ya mafuta, matenki yaongezeke sawia. Tenki liwe na ujazo wa angalau lita 4,500 au 5,000.
Uwe na pampu yenye mkono mmoja au miwili kulingana na aina za mafuta.
(c) Bomba nne (4) za chuma za inchi nne (inchi ) na urefu wa mita tano (mita 5) kwa ajili ya kujengea paa (canopy). Pia, utahitaji bomba za inchi moja au inchi 1.5 na bati kwa ajili ya kenchi na kuezeka (angalia Mchoro Na 2). Bomba za kenchi zinatakiwa kuwa na urefu wa mita saba (mita 7).

Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia wakati wa ujenzi:
(a) Matenki ya kuhifadhia mafuta inabidi yafukiwe ardhini kwa umakini mkubwa. . Kwa sehemu ambazo maji ya ardhini (water table) yapo karibu, ni vizuri matenki yakajengewa zege.

(b) Matenki yapakwe rangi ya kuzuia kutu. Pia, matenki yanatakiwa yafukiwe na mchanga kwa ajili ya kuzuia kutu.

(c) Kituo kinatakiwa kisakafiwe kwa zege imara la angalau inchi nne (inchi 4). Eneo mahsusi la kusakafia ni eneo linalozunguka pampu na eneo la kushushia mafuta (angalia Mchoro Na 1). Eneo linalozunguka pampu liwe na ukubwa wa angalu mita za mraba 45 (yaani upana mita 6.4 na urefu mita 7). Eneo la kushushia mafuta linatakiwa liwe na ukubwa wa angalau mita za mraba 16 (yaani upana mita 4 na urefu mita 4) ili gari la mafuta liweze kusimama kwenye zege hiyo wakati wa kushusha mafuta.

(d) Eneo linalozunguka pampu na eneo la kushushia mafuta ijengewe mitaro inayoelekea kwenda kwenye chemba ya kuchuja mafuta na maji (Oil/water separator). Chemba ya kuchuja mafuta na maji inatakiwa iwe na vyumba vitatu. Kila chumba kiwe na urefu wa mita moja (mita 1), upana mita mbili (mita 2) na kina mita moja (mita 1). Chemba ifunikwe na mifuniko iliyotengenezwa na bati au kichanja imara kilichotegenezwa na nondo. Usitumie zege, ili iwe rahisi wakati wa kusafisha (angalia Mchoro Na 3).

(e) Kituo kinatakiwa kiwe na paa imara (canopy) kama inavyoonyesha kwenye Mchoro Na 2. Paa linatakiwa kuwa na urefu wa mita 5.

(f) Ni vyema kutumia wahandisi wa ujenzi au mafundi wenye uzoefu wa ujenzi wa vituo vya mafuta.

3 Kanuni za EWURA za ujenzi wa vituo vijijini
EWURA imeandaa Kanuni mahsusi kwa ajili ya ujenzi na biashara ya vituo vya mafuta vijijini. Kwa mujibu wa kanuni hizo, mtu yeyote anayetaka kujenga kituo kijijini ni lazima kabla ya kuanza ujenzi apate kibali cha EWURA, baada ya kutuma maombi ya kupewa kibali hicho. Pia, kabla ya kuanza biashara, mwekezaji anatakiwa kuwa na leseni ya EWURA, ambayo hutolewa baada ya EWURA kupokea maombi yaliyozingatia mahitaji yote. Baada ya hapo, EWURA itakagua kituo husika ili kujiridhisha kuwa kinakidhi viwango.

Mchoro Na 1: Ramani ya Kituo cha mafuta inayoonyesha tenki, pampu, ofisi, barabara ya kuingia na kutoka kituoni.

Mchoro Na 2: Picha ikionyesha paa la kituo (canopy).

Mchoro Na 2: Chemba ya kuchuja mafuta na Maji (Oil/Water Separator)

Mchoro Na 3: Picha namna chemba ya kuchuja mafuta na Maji (Oil/Water Separator) inavyotakiwa kujengwa. Chemba ifunikwe na mifuniko iliyotengenezwa na bati au kichanja imara kilichotegenezwa na nondo.

UNAWEZA PIA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Share This

Tags: , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *