LIVE AL AHLY VS WYDAD AC Download HAPA kutazama LIVE kwenye Simu Yako Leo Saa 3:00 Usiku. 

Feisal agonga mwamba tena ombi la Kuvunja Mkataba na Yanga

Filed in Michezo, New by on 05/05/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

Feisal agonga mwamba tena ombi la Kuvunja Mkataba na Yanga

Feisal agonga mwamba tena ombi la Kuvunja Mkataba na Yanga,Feisal Salum Abdallah Yanga SC,Feisal agomewa tena TFF, maamuzi ya TFF ishu ya Feisal Salum na Yanga,hukumu ya TFF ishu ya Feisal Salum Abdallah na Yanga.

Feisal agonga mwamba tena ombi la Kuvunja Mkataba na Yanga

OMBI la kiungo timu ya Taifa ya Tanzania na Young Africans, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ kuvunja mkataba na klabu yake ya Yanga kwa mara nyingine limegonga mwamba mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake Mei 4, 2023 pamoja na mambo mengine ilisikiliza pia shauri la mchezaji Feisal Salum aliyewasilisha malalamiko akitaka kuvunja mkataba wake na Klabu ya Young Africans kupitia barua yake ya tarehe Machi 6, 2023.

Feisal agonga mwamba tena ombi la Kuvunja Mkataba na Yanga,Feisal Salum Abdallah Yanga SC,Feisal agomewa tena TFF, maamuzi ya TFF ishu ya Feisal Salum na Yanga,hukumu ya TFF ishu ya Feisal Salum Abdallah na Yanga.Awali, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilisikiliza malalamiko hayo kwa njia ya maandishi ambapo pande zote (Young Africans SC na Feisal Salum) ziliwakilishwa na wanasheria wao ambao walipewa pia muda wa nyongeza wa kufafanua walichowasilisha kwenye majumuisho yao ya maandishi.

Baada ya kupitia na kutafakari kwa kina hoja zote za pande husika, Kamati imetupilia mbali maombi hayo kwa msingi kwamba ilishaamua juu ya uhalali wa Mkataba wa Mchezaji huyo na klabu yake kwamba ana Mkataba unaoendelea mpaka 2024.

Kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinazotawala uvunjaji wa mikataba ya wachezaji inayoendelea, mchezaji ni lazima aanze na majadiliano na Klabu yake ambayo ndio yenye haki nae imeeleza TFF.

Aidha TFF imesema kuwa uamuzi kamili kwa pande zote mbili zilizokuwa zinahusika katika shauri hilo utatolewa baadae kwa pande husika kujulishwa.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags: , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *