Nijuze Habari

HERSI Rais mpya Yanga SC

Filed in Michezo by on 09/07/2022 0 Comments

Hersi Said Rais mpya Yanga SCMgombea pekee wa nafasi ya urais wa Klabu ya Yanga SC, Injinia Hersi Said amechaguliwa na wanachama baada ya kuridhia kwa kupiga kura za ndio.

Nijuze Habari Application

HERSI Rais mpya Yanga SC

Hersi Said Rais mpya Yanga SCMgombea pekee wa nafasi ya urais wa Klabu ya Yanga SC, Injinia Hersi Said amechaguliwa na wanachama baada ya kuridhia kwa kupiga kura za ndio.

Mwenyekiti Kamati ya uchaguzi Mchungahela kwa mujibu wa ibara ya 23(9) ya kanuni za uchaguzi ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) inasema mgombea akiwa mmoja mkutano Mkuu unapitisha azimio la mgombea kuwa Rais.

Hersi Said Rais mpya Yanga SC“Wajumbe mnaridhia Hersi Said kuwa Rais wa Klabu ya Yanga,” amesema Mchungahela huku wajumbe wakiitikia ndio.

WASHINDI wa tuzo za Ligi Kuu (NBC & TFF AWARDS 2022

Mchungahela amerudia mara tatu kauli hiyo wajumbe wakionekana kumkubali.

Baada ya kupiga kura hizo za wazi za ndio Mchungahela amemtangaza rasmi kuwa Rais wa klabu hiyo.

Wajumbe hao walianza kuimba Hersi Hersi ikamlazimu kupanda jukwani na kuwapungia mikono ikiwa ishara ya shukrani kwa kumuamini.

Hersi Said Rais mpya Yanga SCKabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Klabu hiyo, Eng. Hersi Said alitoa Vipaumbele vyake endapo atakuwa Raisi wa Yanga SC, ambavyo ni;

MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumamosi July 09,2022

1:Miundombinu Ya Klabu
A.Ujenzi wa uwanja wa mechi wenye uwezo wa kubeba watu 20,000 – Kaunda Jangwani

B.Marekebisho ya jengo la klabu – Jangwani

C.Kuendeleza Training Centre – Kigamboni

2:Mabadiliko ya Muundo wa Klabu.
Klabu kupitia kwa wanachama walipitisha mfumo wa mabadiliko, nikiwa mmoja waumini wa mabadiliko hayo, naahidi kuyasimamia na kuyaendeleza mabadiliko hayo kwa mujibu wa Katiba ya Klabu.Hersi Said Rais mpya Yanga SC

3:kuimarisha uchumi wa Klabu.
-Kupitia kwa miradi ya usajili wa wanachana.
-Kupitia kwa miradi ya usajili wa washabiki
-Kuvutia Wadhamini mbali mbali.
-Kuvutia wawekezaji.

4:Kujenga Kikosi imara cha kuleta Mataji na furaha Kwa wana Yanga.
A.Ligi Kuu
B.FA Cup
C.Ngao Ya Jamii
D.Mashindano Ya Kimataifa

Matokeo Kidato cha Sita 2022/2023 Hapa

5:Kujenga timu imara za Vijana na Wanawake.
A.U-17
B.U-20
C.Yanga Princess

6.Kuongeza ushirikiano baina ya Klabu na wanachama na mashabiki wake, wadau mbali mbali ikiwemo idara za serikali, sekta binafsi, waandishi wa habari na watanzania kwa ujumla.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.