Nijuze Habari App

Historia ya Wilaya ya Karagwe

Filed in Makala by on 11/03/2023 0 Comments
Share This

JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA


JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA


AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Historia ya Wilaya ya Karagwe

Historia ya Wilaya ya Karagwe, Historia ya mkoa wa kagera,Kata za wilaya ya karagwe,Halmashauri ya wilaya ya Karagwe,Ramani ya wilaya ya karagwe,Ramani ya kagera na wilaya zake,Historia ya chifu rumanyika,NAFASI ZA KAZI wilaya ya Karagwe,Historia ya wilaya ya kyerwa,Makabila ya kagera,Vijiji vya wilaya ya karagwe,Mkurugenzi wa karagwe,Kagera Tanzania,Historia ya chifu rumanyika,Vijiji vya wilaya ya kyerwa,NAFASI ZA KAZI wilaya ya Karagwe.

Historia ya Wilaya ya Karagwe

CHIMBUKO/ASILI YA KARAGWE NA WATU WAKE (WANYAMBO)

Kutokana na simulizi za wazee na watafiti mbalimbali kama vile Katoke (1975; 162) jina ‘Karagwe jina linatokana na kilima kinachopatikana Kusini Magharibi ya Makao Makuu ya wilaya ya Karagwe ,kwenye kijiji cha Kandegesho ,kata ya Nyakakika ambacho mtawala ( Omukama ) wa kwanza alifanya kafara ya kwanza.

Kwa taarifa zilizopo ni kwamba mtawala huyo alijulikana kwa jina la ‘Nono ya Malija’ kutoka ukoo wa Basiita. Na kwamba kumbukumbu hii ya “Karagwe ka Nono “inatokana na ukweli kuwa Nono alikuwa mtawala wa mwisho wa wenyeji asilia kabla ya kuondolewa madarakani na Omukama Ruhinda mtoto wa Wamara.

Inasemekana kwamba Nono aliondolewa kwa Ujanja bila ya Misukosuko wala mapigano ya aina yoyote. Kwa kifupi hii ndio kumbukumbu yake na chimbuko la Historia ya jina Karagwe.

MIPAKA YA WILAYA.

Wilaya ya Karagwe ni kati ya Wilaya saba (7) za Mkoa wa Kagera.

Wilaya ya Karagwe inapakana na Wilaya ya Kyerwa upande wa Kaskazini, nchi ya Rwanda upande wa Kusini Magharibi, Wilaya ya Ngara upande wa Kusini na Wilaya za Missenyi, Bukoba Vijijini na Muleba upande wa Mashariki.

JIOGRAFIA YA WILAYA YA KARAGWE

Wilaya ipo kilomita 105 kutoka Manispaa ya Bukoba –Makao makuu ya Mkoa wa Kagera. Wilaya inapatikana kati ya nyuzi 1o na 2o, 20′ Kusini Latitudo 30o hadi 38,30 Mashariki Longitudo.

Mwinuko wa ardhi kutoka usawa wa bahari ni mita 1,500 hadi mita 1,800. Hali ya hewa kwa ujumla ni joto la wastani wa degree 26oC. Mvua zinanyesha kwa wastani wa mm 1,040 hadi 1,200 kwa mwaka, kati ya mwezi September na January na kati ya mwezi March na mwezi May.

ENEO LA WILAYA YA KARAGWE

Wilaya ya Karagwe ina eneo la kilomita za mraba 4,500 kati ya hizo kilomita za mraba 4,342 ni eneo la nchi kavu na kilomita za mraba 158 ni eneo la maji.

Eneo linalofaa kwa kilimo ni Hekta 153,540 na eneo linalolimwa ni Hekta 82,808.5 sawa na asilimia 53.9.

UTAWALA.

Kwa upande wa maeneo ya utawala, Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ina Tarafa tano (5) ambazo ni Bugene, Nyakakika, Nyaishozi, Nyabiyonza na Kituntu.

Pia wilaya ya Karagwe ina kata 23, vijiji 77 na vitongoji 612 ambapo kati ya vitongoji hivyo 612, vitongoji 20 vipo katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kayanga na vinaitwa vitongoji kwa sababu bado mamlaka hiyo ya mji mdogo haijawa mamlaka kamili ili vitongoji hivyo viitwe mitaa.

Halmashauri ya wilaya ina waheshimiwa madiwani 32 ambapo kati yao 23 ni wa kuchaguliwa kutoka katika kata za Halmashauri ya Wilaya, 8 ni wa viti maalum na mbunge wa Jimbo 1.

Historia ya Wilaya ya Karagwe, Historia ya mkoa wa kagera,Kata za wilaya ya karagwe,Halmashauri ya wilaya ya Karagwe,Ramani ya wilaya ya karagwe,Ramani ya kagera na wilaya zake,Historia ya chifu rumanyika,NAFASI ZA KAZI wilaya ya Karagwe,Historia ya wilaya ya kyerwa,Makabila ya kagera,Vijiji vya wilaya ya karagwe,Mkurugenzi wa karagwe,Kagera Tanzania,Historia ya chifu rumanyika,Vijiji vya wilaya ya kyerwa,NAFASI ZA KAZI wilaya ya Karagwe.

Historia ya Wilaya ya Karagwe

IDADI YA WATU.

Kulingana na Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Wilaya ya Karagwe ilikuwa na jumla ya watu wapato 332, 020.

Kati ya hao 163,864 (wanaume) na 168,156 (wanawake), ambapo ongezeko la watu ni asilimia 2.9 kwa mwaka.

Maoteo ya watu kwa mwaka 2015 ni kuwa Wilaya ilikuwa na watu 351,555. Kati ya hao, wanawake ni 178,050 na wanaume ni 173,505.

 

MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.

 
 

Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.

 

Aidha idadi ya kaya nayo imeongezeka toka kaya 72,836 mwaka 2012 hadi kaya 76,425 mwaka 2015.

SHUGHULI ZA KIUCHUMI WILAYANI KARAGWE:

1. KILIMO, USHIRIKA NA UMWAGILIAJI:

Kilimo ni mojawapo ya shughuli za kiuchumi inayochangia wastani wa asilimia 70 ya pato la Halmashauri. Kaya zinazoshiriki katika shughuli za kilimo ni 61,351 kati ya kaya zote 76,425 za wilaya ya Karagwe.

Eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 153,540 kati ya hekta 4,500,000 ya eneo lote la wilaya. Eneo linalofaa kwa kilimo cha Umwagiliaji ni hekta 4,500 Pia Wilaya inashirikiana na wadau mbalimbali waliopo wilayani katika kuendeleza sekta ya kilimo.

Baadhi ya wadau hao ni ELCT, Karagwe Agribusiness, MAVUNO, CHEMA, WORLD VISION, MATUNDA MEMA, BISHESHE WINE, KARAGWE ESTATE LTD, RADIO KARAGWE, RADIO FADECO, LUKALE WINE, KDCU, Matunda MEMA, KADERES NA OLAM.

Aidha zipo SACCOS 31 zenye jumla ya wanachama 46,319 na Chama 1 kikuu cha Ushirika (KDCU) kinachojishughulisha na ununuzi wa mazao ya wakulima.

Wilaya imeanzisha na kujenga mradi mmoja mkubwa wa Umwagiliaji (Mwisa Irrigation Scheme) wenye ukubwa wa Hekta 120.

Uhamasishaji wa wananchi kulima mpunga na mbogamboga unaendelea. Mradi huu utaongeza kipato cha mkulima wa Karagwe na kupunguza umaskini.

2. UFUGAJI NA UVUVI:

Wilaya ya Karagwe ina hekta 140,000 zinazofaa na hutumika kwa shughuli za ufugaji. Sekta hii uchangia kwa zaidi ya 10% katika ajira ya wananchi na pato la kaya. Mifugo ambayo hufugwa ni pamoja na ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku, bata na sungura.

Shughuli za Uvuvi ufanyika katika maziwa madogo ya Burigi, Rwakajunju, Kamakala na mto Kagera. Wilaya inayo mabwawa ya kuchimbwa 67 kwa ajili ya ufugaji wa samaki.

Uzalishaji wa samaki ni wastani wa kilo 33,000 kwa mwaka. Aina za samaki wanaozalishwa kwa wingi ni sato/ngege, kambale mamba, kambale mumi, furu, ningu, soga na domodomo.

3. VIWANDA NA BIASHARA:

Mji wa Kayanga na Omurushaka pamoja na miji midogo ya Kihanga, Nyakaiga, Rwambaizi, Nyaishozi, Chanyamisa, Nyabiyonza, Nyakabanga na Ihembe ni kati ya miji inayokua kibiashara na yenye mwingiliano mkubwa wa shughuli za kiuchumi na kijamii.

Maeneo haya yanaendelea kuwekeza katika viwanda vya biashara kama vile viwanda vya kukoboa Kahawa, viwanda vya kusindika maziwa, asali, kusaga na kukoboa nafaka. Shughuli za uzalishaji zinaendelea kuimarika na kuongeza uzalishaji, kupanua ajira, kukuza biashara ya uuzaji na ununuzi wa mazao tarajiwa na hivyo kuongeza kipato na kukuza uchumi, kuboresha maisha ya jamii, kupunguza umaskini wa kipato na hivyo kuchochea kasi ya kuondoa umaskini.

WATAWALA WA KARAGWE

Watawala wa Karagwe walikuwa na cheo cha “Umugabe”. Nasaba ilianzishwa mnamo mwaka 1450 na mtemi Ruhinda I aliyeitwa pia Bunyambo.

1675 – 1700 Ruhinda V

1700 – 1725 Rusatira

1725 – 1750 Mehinga

1750 – 1775 Kalemera I Ntagara Bwiragenda (alifariki 1775)

1775 – 1795 Ntare V “Kiitabanyoro”

1795 – 1820 Ruhinda VI Orushongo “Lwanyabugondo” (b. 1777 – d. 1820)

1820 – 1853 Ndagara I “Luzingamcucu lwa nkwanzi”

1853 – 1881 Rumanyika I Rugundu

1882 – 1886 Ndagara II Nyamkuba

1886 – 1893 Kalemera II Kanyenje

1886 – 1893 Kakoko -Regent

1893 – 1914 Ntare VI

1914 – 1916 Kahigi -Regent

1916 – 1939 Daudi Rumanyika II

1939 – 1962 – 9.12. B. Itogo Ruhinda VII

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Share This

Tags: , , , , , , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *