IGP Wambura afanya Mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa May 2023

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


IGP Wambura afanya Mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa May 2023

IGP Wambura afanya Mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa May 2023
MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillius Wambura amefanya Mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa kwa kuwahamisha na wengine kupangiwa majukumu mengine.
Mabadiliko hayo yamefanyika Jana May, 15, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Jeshi hilo Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi Dodoma, David A.Misime- SACP amesema katika Mabadiliko hayo IGP Camillius Wambura amemhamisha Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Longinus Alexander Tibishibwamu (RPC) kwenda Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
Nafasi ya ACP Longinus inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Salum Ramadhani Morcase ambaye alikuwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
Pia amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Geofrey Sarakikya kwenda Makao makuu ya Polisi Dodoma.
Nafasi ya Sarakikya inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Michael Njera ambaye alikuwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
Msemaji huyo wa Jeshi la Polisi amesema aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Hamis Issah amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelekezi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Makuri Imori.
David amesema aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu amehamishiwa mkoa wa Kagera kuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa huo na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Edith Swebe.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Willium Mwampagale amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Pemba.
IGP Wambura afanya Mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa May 2023, Mkuu wa polisi mpya,Kamanda wa polisi dar es salaam,Orodha ya makamanda wa polisi tanzania, Makamanda wa polisi mikoa,Wakuu wa polisi wa mikoa.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- TETESI za Usajili NBC Premier League 2023/2024
- YANGA yashika Nafasi ya 9 Simba ya 10 Afrika 2022/2023
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: IGP Wambura afanya Mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa May 2023, IJP Wambura afanya Mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa May 2023, Kamanda wa polisi dar es salaam, Makamanda wa polisi mikoa, Mkuu wa polisi mpya, Orodha ya makamanda wa polisi tanzania, Wakuu wa polisi wa mikoa.