Nijuze Habari

JEZI kuzinduliwa kabla ya Simba Day

Filed in Michezo by on 05/08/2022 0 Comments

JEZI kuzinduliwa kabla ya Simba DayMeneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amewahakikishia wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kuwa watazindua jezi mpya kabla ya Tamasha la Simba Day litakalofanyika Jumatatu, August 08,2022.

Nijuze Habari Application

JEZI kuzinduliwa kabla ya Simba Day

JEZI kuzinduliwa kabla ya Simba DayMeneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amewahakikishia wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kuwa watazindua jezi mpya kabla ya Tamasha la Simba Day litakalofanyika Jumatatu, August 08,2022.

Ahmed amewaomba radhi Wanasimba kwa changamoto hiyo iliyojitokeza lakini amewahakikishia jezi zitakuwa sokoni ndani ya saa 48 zijazo.

“Nakiri hili sio jambo la kawaida kwani tulipaswa kuwa tayari tumezindua jezi zetu lakini kulikuwa na changamoto kidogo iliyosababishwa na kubadilika kwa Mdhamini Mkuu

“Niwahakikishie wapenzi na wanachama wetu kuwa tutazindua jezi kabla ya Jumatatu, ndani ya siku hizi mbili jezi zitakuwa hadharani, alisema Ahmed

Aidha Ahmed amekanusha uzushi unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa jezi hizo zimezuiwa bandarini kutokana na kutolipiwa ushuru.

“Nenda kazunguuke makontena yote hapo bandarini hutaona jezi za Simba, huo ni uzushi tu, Wanasimba watulie, jezi zao zipo tayari kuna mambo madogo tunaweka sawa”

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.