JINSI ya Kujibu Maswali Yanayoulizwa kwenye Usaili
JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA
JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA
AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
JINSI ya Kujibu Maswali Yanayoulizwa kwenye Usaili

JINSI ya Kujibu Maswali Yanayoulizwa kwenye Usaili
USAILI wa ajira (job interviews) husababisha hofu na msongo wa mawazo kwa vijana wengi kabla au baada ya kutoka chumba cha usaili.
Tatizo hilo hutokana na hofu inayojenga wakati wa kujibu maswali unayoulizwa na watu ambao wamekuzunguka wakati wa kufanyiwa usaili.
Wanataaluma vijana ambao kwa mara ya kwanza wanaitwa kwenye usaili wa ajira hushindwa kujieleza au kujibu maswali ipasavyo, yanayoulizwa kwa msingi wa kutaka kujua uwezo wako kwa namna moja au nyingine.
Kujibu maswali ya usaili hakuhitaji ‘mbwembwe’ nyingi – kuwa mjuaji au maelezo, isipokuwa waajiri huhitaji majibu ya wazi na mafupi yenye mvuto, ambayo hayaleti maswali mengine kwa mwaajiri.
Wataalamu wa ajira walijaribu kuangalia baadhi ya maswali ambayo ukifanikiwa kujibu kama ipasavyo, utakuwa kwenye nafasi kubwa ya kumshawishi mwajiri kukupa nafasi moja kwa moja.
Hii ni baadhi ya mifano ya maswali na majibu yenye ushawishi mkubwa kwa mwajiri, ambayo ukiweza kuyajibu kwa kujiamini utapata ajira bila kutoka jasho la hofu.
Maswali 15 Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kwenye Usaili (Interviews) na Namna ya Kuyajibu
1:JITAMBILISHE (Wewe ni nani?)
Mara nyingi hili ni swali ambalo mtahiniwa huulizwa mara tu aingiapo kwenye chumba cha usaili.
Kwa bahati mbaya watahiniwa wengi hudhani kuwa waajiri hutamani kujua majina yao. Hapana, majina yako wanayafahamu na pengine hata taarifa za ziada.
Katika swali hili waajiri uhitaji kujua sifa zako zihusianazo na ajira zitakazo dhihirisha kuwa wewe ni mtu sahihi.
Mfano mtu anaweza kujibu hivi, “Jina langu ni Mti Mkavu Amon Amos, ni Mhitimu wa Shahada ya Masoko ya Chuo Kikuu Dodoma.
Ni mtu makini, mbunifu, mchapa kazi na ninayependa watu. Pamoja na hayo ninao ujuzi usio na shaka kwenye masuala ya mawasiliano.
Uwezo wangu unadhihirishwa na mrejesho ambao huwa naupata kwa kila mtu ninaye fanya naye kazi”.
Katika swali hili ni muhimu kujua kuwa halihitaji wewe kuzungumzia mambo yasiyo husiana na kazi na ajira.
Kwenu mpo wa ngapi, jina la mama yako, mkoa unaotoka, kabila, kazi ya Baba au Mama yako havihitajiki katika taarifa unazotakiwa.
2:KWANINI UPEWE AJIRA KWETU?
Au unaweza ukaulizwa Kwa nini unahisi wewe ni mtu sahihi kwa kazi hii na siyo mwingine? Kumbuka kuwa usaili wa kazi unahusisha ushindani hivyo swali hili linataka uoneshe utofauti ulionao. Katika kujibu swali hili zingatia mahitaji ya kazi husika kujenga hoja kwani hata kama una utofauti wa aina gani kama hautasaidia katika kufikia malengo ya taasisi bado itakuwa ni kazi bure.
Mfano, “ Siyo kwamba mimi ni mchapakazi na mbobezi katika uhasibu pekee lakini pia ni mtu ambaye ninaweza kufanya shughuli zangu bila kusimamiwa. Mimi ni mtu wa matokeo hivyo kwa kila ambacho hufanya hulenga kutimiza malengo kwa wakati na kufikia viwango stahiki.
“Ubora wangu unathibitishwa na tuzo kadhaa nilizowahi kupata ikiwemo mfanyakazi bora wa mwezi mara nne nilipokuwa nikifanya kazi na na Magogo Media. Hii inathibitisha kuwa mkinipa fursa hii hamtakuwa mnajaribu bali mtakuwa mnafanya maamuzi sahihi”.
3. UNAJUA NINI KUHUSU SISI?
Siku zote maandalizi ya usaili yanaenda sambamba na kutafuta taarifa sahihi za taasisi husika. Hivyo ni vyema kuhakikisha kuwa taarifa unazotoa hapa ni sahihi na muhimu katika kudhirisha kuwa ulishafanya utafiti wa kutosha kuhusu taasisi husika.
Mfano, “ Benki yenu ilianzishwa mwaka 1987 ina maono ya kuwa benki bora kuliko zote nchini kwa kutoa huduma za kifedha zinazo aminika na kufikia maeneo mengi nchini. Kwa sasa benki yenu ina matawi 700 na ATMs 500 huku ikiwa na mpango wa kufungua matawi mengine Kigoma hivi karibuni.
Endapo mtanipa fursa ya kufanya kazi na nyinyi nitahakikisha natumia vyema uwezo wangu katika masuala ya masoko ili kuongeza wateja na kuhaikisha huduma bora mnayotoa inafahamika kwa watu wengi.”
4. NI VITU GANI UNAVYOJIVUNIA?
Katika swali hili waajiri huhitaji kujua mambo kadhaa ambayo unayaona kama mtaji mkubwa katika utendaji kazi. Ni vyema kukumbuka kuwa mambo utakayo yataja hapa ni yale yenye umuhimu katika kuongeza ufanisi au ubora katika kazi husika kwani kila kazi inamahitaji yake ya tofauti na kazi nyingine.
Kwa mfano, “mambo makuu mawili ninayojivunia ni ujuzi na uwezo katika huduma kwa wateja na kujisimamia katika majukumu yangu. Kila ninapowahudumia wateja huwa napokea mrejesho chanya juu ya namna wanavyoridhishwa na huduma yangu hivyo kutamani kuhudumiwa nami tena.
Hii hunifanya nijione kuwa mtu muhimu sana katika taasisi yoyote ninayofanya nayo kazi. Pia, uwezo wangu katika kufanya shughuli bila kusimamiwa au chini ya usimamizi mdogo unanifanya niwe mtu wa kuaminiwa na kutegemewa katika kufanya shughuli zangu.Haya ni baadhi ya mambo mengi yanayonifanya mimi kuwa mtu wa tofauti. Nina amini hamtaacha fursa ya kufanya kazi nami”.
5.UDHAIFU WAKO NI UPI?
Hili ni moja ya maswali ambayo watainiwa wengi huyachukia na kuyaona kama yana lengo la kuwatafutia sababu za kuwanyima kazi. Wengine kwa lengo la kuonesha ukamilifu huthubu kusema kuwa hawana udhaifu wowote-usithubutu kusema hivyo. Kila mtu ana udhaifu wake kwani hakuna aliye mkamilifu.
MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.
Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.
Suala la msingi ni kujua namna ya kujibu suali hili. Mambo ya kuzingatia ni pamoja na kuchagua udhaifu ambao hauta athiri utendaji wako na pili hakikisha udhaifu huo unahusiana na ujuzi na sio tabia.
Ujuzi ni rahisi kuutafuata lakini kubadilisha tabia ni ngumu zaidi hivyo usiseme kuwa wewe ni mvivu,mdokozi, na mengineyo ya kitabia. Na unapotaja udhaifu wowote kumbuka kuonesha jitihada ambazo umeshazifanya ili kudhibiti udhaifu huo.
Kwa mfano, kwa kazi ya uhasibu mtu anaweza sema, “Udhaifu nilio nao ni masuala ya ‘graphic designing’ niligundua hili nilipohitaji kuandaa tangazo kwa ajili ya ofisi niliyokuwa nikifanya nayo kazi. Hata hivyo, nimeanza kujifunza mwenyewe kupitia mtandao wa internet na naona napata mabadiliko chanya kila leo”. Kwa jibu hili ni dhahiri kabisa graphic designing siyo mahitaji muhimu ya kazi ya uhasibu hivyo haita athiti utendaji wa kazi.
6. KWANINI ULIACHA KAZI YAKO YA MWANZO?
Hapa unahitajikua makini sana, kumbuka na epuka kuzungumza vibaya kuhusu muajiri yeyote kabla au sasa au uwezo wa muajiri.
Hapa unaweza ukawajibu tu kwamba;” Kwa sababu ya kuboresha na kuongeza ujuzi, pia natafuta fursa bora zaidi.”
7. UNATARAJIA KUPATA NINI KUTOKANA NA KUFANYA KAZI HAPA?
Au unaweza ukaulizwa | Baada ya miaka mitatu wewe mwenyewe utakua wapi? Ongelea unachotumaini kutimiza ila kuwa mkweli. Pia usiongee kwa ujumla. Chagua kitu maalum ambalo ni muhimu kwa kampuni alafu ilenge. Ila, uwe wazi kwa kusema itachukua muda kujifunza zaidi kuhusu kampuni ili kufanikiwa zaidi.
Kwa mfano; “Nikiwa mwalimu wa kiingereza, lengo langu ni kuongeza asilimia ya wanafunzi wanaofaulu mtihani wa taifa kuwa 85% ya darasa yangu. Najua itachukua muda kujua vizuri changamoto za wanafunzi ila, naamini nitafanikiwa”.
Ni vizuri kusema kwamba unatumaini kuona uwajibikaji zaidi katika kampuni hiyo na kuongeza thamani katika kampuni kwa mchango wako.
8. KWANINI UMEKAA MUDA MREFU BILA KUPATA AJIRA?
JIBU kwamba; “Nilikuwa najiendeleza katika taaluma yangu “.
9. ELEZA NAMNA UNAVYOWEZA KUJISIMAMIA MWENYEWE
JIBU kwamba: Nitakuwa nafanya kazi niliyopewa nikishirkiana na wasimamizi wangu na viongozi juu ya namna ya kumaliza kazi kabla ya muda uliopangwa.
10. KITU GANI KINAKUKERA MIONGONI MWA WAFANYAKAZI WENZAKO?
JIBU kwamba; “Naamini katika kufanya kazi kwa pamoja. Hata kama nikikerwa na kitu chochote, huwa najaribu kuepuka isipokuwa kama ni kitu cha binafsi.”
11. UNATEGEMEA KUFANYA KAZI KWA MUDA GANI KAMA UKIPEWA AJIRA?
JIBU:Kwa muda mrefu kama nitaendelea kuongeza kitu katika taaluma yangu.
12:JE, MWENYEWE UNAJIONA UMEFANIKIWA?
JIBU: Ndio, ukiachana na uwezo wa taaluma yangu, nadhani nimepata watu sahihi wa kufanya nao kazi.
13.UWEZO WAKO NI UPI KATIKA KAZI?
JIBU: Mimi huwa naelewa na kufundishika kwa haraka na ni mchapakazi wa kweli.
14. UNAPENDA NAFASI YA CHEO GANI KATIKA TIMU UTAKAYOFANYA NAYO KAZI?
JIBU: Haijalishi hadi nitakapojifunza kitu kipya kwa kila mradi au kazi.
15. JE, UNA SWALI LOLOTE KWETU?
Mwishoni wa interview, ni kawaida kwa mwajiri kuuliza kama una maswali kwao.
Ukipewa nafasi hii, usiulizie mshahara na faida zingine, Badala yake, uliza:
- Maadili ya kampuni
- Aina ya uongozi
- Wafanyakazi wenzako
- Chochote ambacho hukuelewa kuhusu kazi hiyo.
- Watakupa jibu baada ya muda gani?
USIFANYE HAYA MAKOSA KATIKA SWALI HILO:
- Je, kuna fursa ya kukua / kupandishwa ngazi?
- Nitapata siku ngapi za likizo?
- Waajiriwa wanafaidika vipi na kampuni hii.
NB: Tiba bora ya msongo wa interview ni kujiandaa Ingawa interview inaweza ikakupa misongo mingi, ukijiandaa vizuri Utashangazwa na mafanikio yako.
Interview ni nafasi yako ya mwisho kumvutia mwajiri, na vidokezo vilivyoelezwa hapo juu vitakusaidia na hilo.
Kumbuka, hamna haja ya kuwa na wasiwasi ukiwa umejiandaa.
Nakutakia Mafanikio mema kwenye Interview.
Sasa, kwa kuwa umeshajua jinsi ya kujibu vizuri maswali ya Interview, anza kutafuta kazi unayoitaka.
JINSI ya Kujibu Maswali Yanayoulizwa kwenye Usaili, Jinsi ya kueleza historia yako kwa ufupi,Maswali yanayoulizwa kwenye Interview ya Sensa,Maswali yanayoulizwa kwenye usaili wa polisi,Jinsi ya kujitambulisha kwenye usaili,Maswali ya written interview utumishi, Maswali ya interview PDF,Maswali 15 Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kwenye Usaili (Interviews) na Namna ya Kuyajibu
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- TETESI za Usajili NBC Premier League 2023/2024
- YANGA yashika Nafasi ya 9 Simba ya 10 Afrika 2022/2023
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Tags: Jinsi ya kueleza historia yako kwa ufupi, JINSI ya Kujibu Maswali Yanayoulizwa kwenye Usaili, Jinsi ya kujitambulisha kwenye usaili, Maswali 15 Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kwenye Usaili (Interviews) na Namna ya Kuyajibu, Maswali ya interview PDF, Maswali ya written interview utumishi, Maswali yanayoulizwa kwenye Interview ya Sensa, Maswali yanayoulizwa kwenye usaili wa polisi