Nijuze Habari App

Jinsi ya Kupata Leseni ya Udereva (TRA Leseni ya Udereva)

Filed in Makala, Michezo by on 09/04/2023 0 Comments
Share This

SHINDA 50,000 BURE KILA SIKU BONYEZA HAPA


AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Jinsi ya Kupata Leseni ya Udereva (TRA Leseni ya Udereva)

Jinsi ya Kupata Leseni ya Udereva (TRA Leseni ya Udereva), Jinsi ya Kupata Leseni ya Udereva (TRA Leseni ya Udereva) kurenew leseni ya udereva, jinsi ya kuangalia leseni ya udereva, jinsi ya kuangalia leseni yako mtandaoni, bei ya leseni ya udereva, jinsi ya kupata tin number ya udereva, leseni ya udereva

 • Uwe umehudhuria mafunzo katika Chuo chochote kinachofahamika na kupewa cheti
 • Uwe na umri zaidi ya miaka 18 kwa ajili ya gari na umri wa miaka 16 na kuendelea kwa ajili ya pikipiki
 • Uwe na leseni ya kujifunzia/ya muda ya udereva
 • Uwe umelipa ada ya kufanyiwa majaribio – GRR
 • Uwe na cheti cha kupimwa macho
 • Uwe umepeleka maombi kwenye ofisi ya polisi wa usalama barabarani kwa ajili ya kufanyiwa majaribio
 • Uende kwenye ofisi ya polisi wa usalama barabarani  ukiwa na gari kwa ajili ya kufanyia majaribio

Baada ya mwombaji kufanyiwa majaribio anaweza kuruhusiwa kuendesha pikipiki na magari madogo.

 • Mwombaji ataenda kwenye ofisi ya polisi wa usalama barabarani akiwa na leseni yake ya zamani ya udereva
 • lazima awe na cheti cha umahiri
 • mwombaji awe na umri zaidi ya miaka 18 kwa magari na miaka  16 kwa pikipiki

KUBADILI ILI KUPATA DARAJA ”C”

 • Mwombaji ataenda katika ofisi ya polisi wa usalama barabarani akiwa na leseni yake ya zamani ya udereva
 • Awe na cheti cha umahiri
 • Mwombaji awe na umri zaidi ya miaka 18 kwa magari na miaka 16 kwa pikipiki
 • Cheti cha Gari la Kubeba Abiria (PCV) kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji au VETA
 • Mwombaji anatakiwa kubainisha aina ya gari analokusudia kuendesha
 • Mwombaji atapewa daraja la leseni kulingana na mafanikio yake.
 • JINSI ya Kupata TIN namba Online

kwanini ni Muhimu kua na leseni ya udereva

Leseni ya udereva ni muhimu kwa sababu inathibitisha kuwa mtu amepata mafunzo na anao ujuzi unaohitajika kwa usalama na uadilifu wa kuendesha gari. Hapa kuna sababu kadhaa kwa nini leseni ya udereva ni muhimu:

 • Usalama Barabarani: Leseni ya udereva huthibitisha kuwa mtu amepata mafunzo sahihi juu ya sheria za barabarani, ishara za trafiki, na kanuni za usalama. Watu wanaopata leseni ya udereva wamejaribiwa na wameonyesha uwezo wao wa kuendesha gari kwa usalama. Hii inasaidia kupunguza hatari ya ajali barabarani.
 • Kufuata Sheria: Leseni ya udereva inaweka mtu chini ya wajibu wa kufuata sheria za barabarani. Kwa kupata leseni, mtu huzingatia kanuni na sheria ambazo zinapaswa kufuatwa wakati wa kuendesha gari. Hii ni muhimu kwa kuweka nidhamu kwenye barabara na kuwezesha usalama wa watumiaji wengine wa barabara.
 • Utambulisho na Uthibitisho: Leseni ya udereva inatoa utambulisho rasmi na uthibitisho wa uwezo wa mtu wa kuendesha gari. Inaweza kutumika kama hati ya kitambulisho wakati mwingine na inathibitisha kuwa mtu ana ujuzi maalum.
 • Upatikanaji wa Bima: Kampuni za bima za gari mara nyingi zinahitaji leseni ya udereva kama sehemu ya mchakato wa kupata bima ya gari. Leseni ya udereva inathibitisha kwamba mtu ana ujuzi wa kuendesha gari na anaweza kuwa dereva mzuri, ambayo inaweza kupunguza gharama ya bima.
 • Kusaidia Utekelezaji wa Sheria: Leseni ya udereva inasaidia mamlaka za usalama barabarani kufuatilia na kudhibiti madereva. Kwa kuwa kila leseni ina nambari yake ya kitambulisho, inakuwa rahisi kuchunguza madereva wanaofanya makosa au kukiuka sheria na kuwachukulia hatua stahiki.

Ni muhimu kukumbuka kuwa leseni ya udereva ni hati ya kuthibitisha ujuzi wa kuendesha gari kisheria. Ni jukumu la mmiliki wa leseni kuhakikisha kuwa anafuata sheria na kuendesha gari kwa usalama wakati wote.

 

MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.

 
 

Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.

 

Makundi ya leseni za udereva ni yapi?

Mfumo wa leseni za udereva utakuwa na makundi mbalimbali ya madaraja ya leseni za udereva kama ifuatavyo:

Pikipiki

 • A – Leseni ya kuendesha pikipiki zenye/zisizo na kigari na ambazo injini zake zina ukubwa zaidi ya cc 125 au uzito wa kilo 230.
 • A1 – Leseni za kuendesha pikipiki zisizo na kigari na ambazo ukubwa wake wa injini ni mdogo kuliko cc 125 au chini ya kilo 230.
 • A2 – Leseni ya kuendesha pikipiki za magurudumu matatu na manne.
  A3 – Leseni za kuendesha pikipiki baiskeli ambazo ukubwa wake wa injini hauzidi cc 50

Vyombo Binafsi vya Moto

 • B – Leseni ya kuendesha aina zote za vyombo vya moto isipokuwa pikipiki, magari ya biashara, magari makubwa na magari ya kutoa huduma kwa umma.
  Magari ya kutoa huduma kwa Umma
 • C – Leseni ya kuendesha magari ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria 30 na zaidi pamoja na dereva. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo wa juu unaokubalika usiozidi kilo 750.
 • Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja C1 au E kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
 • C1 – Leseni ya kuendesha magari ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria 15 lakini wasiozidi 30, abiria pamoja na dereva. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo wa juu unaokubalika usiozidi kilo 750.
 • Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja D kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
 • C2- Leseni za kuendesha magari ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria wanne lakini wasiozidi kumi na tano.
 • Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo unaokubalika usiozidi kilo 750.
 • Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja D kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
 • C3 – Leseni za kuendesha magari ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria wanne au pungufu akiwemo dereva. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo unaokubalika usiozidi kilo 750.
 • Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja D kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.

Magari Madogo ya Mizigo ya Biashara

 • D – Leseni ya kuendesha aina zote za vyombo vya moto isipokuwa pikipiki, magari makubwa na magari ya kutoa huduma kwa umma.

Magari makubwa ya Mizigo ya biashara

 • E – Leseni ya kuendesha aina zote za vyombo vya moto isipokuwa pikipiki na magari ya umma. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja D kwa muda usiopungua miaka mitatu.

Magari yenye Trela

 • F – Leseni ya kuendesha magari yanayokokota trela.

Magari ya Shambani na Migodini

 • G – Leseni ya kuendesha magari ya shambani na migodini.

Wanaojifunza

 • H – Leseni ya muda ya kujifunza
Viwango vya leseni za udereva ni:
Ada za leseni Shilingi 70,000/= itakayolipwa kila baada ya miaka 5
Ada ya jaribio la kuendesha Shilingi 3,000/=
Ada za leseni ya muda Shilingi 10,000/= itakayolipwa kila baada ya miezi 3

KWA MAELEZO/HUDUMA ZAIDI UNAWEZA KUFIKA KATIKA OFISI YA TRA ILIYOKARIBU NAWE.

leseni ya udereva 2023,namba ya leseni ya udereva,jinsi ya kuangalia leseni ya udereva,jinsi ya kupata leseni ya udereva online.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Share This

Tags: , , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *