JINSI ya Kurasimisha/Kuhakiki namba za ziada ulizosajili kwa NIDA yako

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


JINSI ya Kurasimisha/Kuhakiki namba za ziada ulizosajili kwa NIDA yako

JINSI ya Kurasimisha/Kuhakiki namba za ziada ulizosajili kwa NIDA yako
Kampeni ya kuhakiki Namba za Simu inamtaka kila mtumiaji wa huduma za Mawasiliano ya simu, kuhakiki namba yake iliyosajiliwa kwa namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
Kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta (EPOCA) 2010, ni kosa Kisheria kutumia laini ya simu ambayo haijahakikiwa hivyo kila Mwananchi anatakiwa kuhakiki laini yake iliyosajiliwa kwa namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) ili kuepuka kufungiwa laini yake.
Ili kuhakiki namba yako bonyeza/bofya *106#, chagua namba 5 kisha namba 1 kuhakiki namba kuu. Kama una namba zaidi ya moja, rudia tena zoezi hilo kwa kubofya/kubonyeza *106#, chagua namba 5 kisha chagua namba 2 kuhakiki namba za ziada.
Kupata maelezo zaidi yakuhakiki namba yako/zako; tafadhali, tembelea duka au wakala wa Mtoa Huduma wako.
Kumbuka Laini zote ambazo zitakuwa hazijahakikiwa baada ya February 13, 2023 saa 10 jioni zitafungwa
Kama unapata changamoto ya kuhakiki namba yako ya simu kwa sababu ulisajili kwa Kitambulisho cha Taifa cha mtu mwingine, basi tembelea Ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili upate namba utambulisho yaani National Idenfitification Number (NIN) itakayokuwezesha kukamilisha usajili wako.
Hatua za kufuata ili kuhakiki laini zako zilizosajiliwa kwa namba ya Kitambulisho cha Uraia/Taifa au NIDA.
Kwenye simu yako Bofya *106# (kisha bonyeza kitufe cha kupiga simu kwa mtandao husika;
Menyu itajitokeza kwenye skrini ya kifaa chako cha mawasiliano ikiwa na vipengele vitano (5), Menyu hii inafanana kwa mitandao yote.
Ikiwa una namba moja pekee kwa Mtandao husika, unashauriwa kuhakiki kama namba yako ya Kitambulisho cha Uraia ilitumika kusajili namba hiyo pekee, au namba nyingine usizozitambua.
Kutekeleza zoezi hili chagua kipengele cha Tatu (3) kwenye menyu inayoonekana kwenye skrini ya kifaa chako.
Iwapo utabaini uwepo wa namba za simu usizozitambua fika kwenye duka la Mtoa Huduma wako, ili uzifute.
Hakikisha unacho kitambulisho chako cha Uraia au namba ya utambulisho (NIN) ili kukamilisha zoezi hili.
Ikiwa unamiliki namba zaidi ya moja za mtandao mmoja zilizosajiliwa kwa namba ya kitambulisho chako cha Uraia (NIN) unapaswa kuzihakiki.
Kutekeleza zoezi hili, chagua kipengele cha Tano (5) kwenye menyu iliyotokeza kwenye skrini ya kifaa chako. Kisha, bofya kipengele namba (1) ili kuchagua Namba Kuu. halafu, rudia kwa kubofya kipengele namba (2) kuhakiki namba za ziada.

Piga *106#, chagua 5 kisha chagua 1 kuhakiki namba kuu au chagua 2 kuhakiki namba za ziada.
Hakiki Leo. Piga *106#, chagua 5 kisha chagua 1 kuhakiki namba kuu au chagua 2 kuhakiki namba za ziada.
Pia unaweza kutembelea duka au Wakala wa mtandao wako kuepuka laini kufungiwa.
Faida za kuhakiki laini zako zilizosajiliwa kwa Kitambulisho cha Uraia ni kama ifuatavyo;
-Uhakiki unakuhakikishia Usalama wako wewe kama mtumiaji wa huduma za Mawasiliano ya simu.
-Ni utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) na Kanuni zake zinazoelekeza kwamba laini zote zisajiliwe kwa utaratibu bayana.
-Zoezi hili litawezesha kuondoa kwenye ikolojia ya Mawasiliano simu-laghai zinazosababisha matukio ya uhalifu miongoni mwa watumiaji wengine wa huduma za Mawasiliano ya simu.
-Uhakiki unakupa utambulisho thabiti (Digital identity). Unakuwezesha wewe Mwananchi kuwa mshiriki Madhubuti katika Ujenzi wa uchumi wa Taifa lako (Uchumi wa Kidijitali).
-Kuboresha Huduma. Taarifa za watumiaji zilizokamilika zinaiwezesha Serikali kupitia TCRA kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za Mawasiliano.
Kila mtumiaji wa Mawasiliano ya simu nchini, aliekidhi vigezo vya kuwa na kitambulisho wa uraia anapaswa kwa mujibu wa kanuni za usajili wa laini za simu, kusajili na kuhakiki laini zake kwa utambulisho wake husika.

Piga *106#, chagua 5 kisha chagua 1 kuhakiki namba kuu au chagua 2 kuhakiki namba za ziada.
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
DONWLOAD NIJUZE TV HAPA SISI kwetu Michezo ndiyo Furaha YETU.
JINSI ya Kurasimisha/Kuhakiki namba za ziada ulizosajili kwa NIDA yako
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: Jinsi ya kufuta usajili wa laini zako, Jinsi ya kuhakiki namba ya simu vodacom, Jinsi ya kujua namba yako ya simu, Jinsi ya kurasimisha namba ya simu Airtel, Jinsi ya kurasimisha namba ya simu Halotel, Jinsi ya kurasimisha namba ya simu Tigo, Jinsi ya kurasimisha namba ya simu TTCL, Jinsi ya kurasimisha namba ya simu vodacom, JINSI ya Kurasimisha/Kuhakiki namba za ziada ulizosajili kwa NIDA yako, Kuangalia namba zilizosajiliwa NIDA yako, Kurasimisha ni nini