JINSI ya kuweka akaunti ya WhatsApp Business kwenye Ukurasa wa Facebook
JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPPÂ HAPA
JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA
AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
JINSI ya kuweka akaunti ya WhatsApp Business kwenye Ukurasa wa Facebook

JINSI ya kuweka akaunti ya WhatsApp Business kwenye Ukurasa wa Facebook
Unapotumia programu ya WhatsApp Business, unaweza kuunganisha Ukurasa wako wa Facebook na akaunti yako ya WhatsApp Business.
Kidokezo cha Biashara: Kuunganisha akaunti yako ya WhatsApp Business kunawawezesha wateja wanaotembelea Ukurasa wako wa Facebook kukutumia ujumbe moja kwa moja kwenye WhatsApp kwa kubofya mara moja tu.
Ili kuunganisha akaunti hizi na kuwezesha usawazishaji, lazima uwe na yafuatayo:
- Ukurasa wa Facebook kwaajili ya biashara yako.
- Akaunti kwenye programu ya WhatsApp Business.
- Matoleo ya hivi karibuni ya programu za vifaa vya mkononi.
Kuunganisha akaunti yako ya WhatsApp Business na Ukurasa wa Facebook
Unaweza kuunganisha akaunti zako kutoka kwenye programu ya WhatsApp Business.
- Fungua programu ya WhatsApp Business.
- Kwenye Android, gusa Chaguo zaidi, kwenye iPhone, gusa Mipangilio
- Gusaa Zana za Biashara > Facebook na Instagram.
- Gusa Facebook > ENDELEA. Itafungua ukurasa wa kuingia kwenye Facebook.
- Weka maelezo ya kuingilia kwenye akaunti yako ya Facebook. Gusa Ingia.
- Chagua Ukurasa wa Facebook unaotaka kuunganisha na akaunti yako ya WhatsApp Business, Gusa Unganisha WhatsApp.
- Ikiwa huna ukurasa wa Facebook, utapewa chaguo la kufungua.
- Sasa utaona Kitufe cha WhatsApp kwenye ukurasa wako wa Facebook.
- Mara unaporudi kwenye programu ya WhatsApp Business, utaona ukurasa wako wa Facebook uliounganishwa upande wa juu ya skrini ya Facebook na Instagram.
- Kusawazisha taarifa zako za biashara kwenye Facebook na WhatsApp
- Unaposawazisha akaunti zako, mabadiliko yoyote unayofanya kwenye taarifa za biashara katika ukurasa wako wa Facebook zitaonekana kiotomatiki kwenye jalada lako la WhatsApp Business.
Usawazishaji huu unafanya kazi kuelekea upande mmoja tu, kutoka kwenye Ukurasa wako wa Facebook kwenda kwenye programu ya WhatsApp Business.
Kwa mfano: ukijaribu kubadilisha saa za biashara kwenye programu ya WhatsApp Business, utapata ujumbe wa onyo kuwa usawazishaji utakomeshwa.
Ukiendelea kuhariri saa zako za kazi, akaunti yako ya WhatsApp Business itaonyesha saa mpya na Ukurasa wako wa Facebook utaonyesha saa za zamani.
MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.
Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.
Kumbuka: Mara tu usawazishaji unapoanzishwa, utafanya kazi kwenye wavuti na simu.
Kuondoa akaunti yako ya Facebook iliyounganishwa kwenye programu ya WhatsApp Business
Ikiwa hutaki tena akaunti zako ziwe zimeunganishwa, unaweza kutenganisha akaunti yako ya Facebook na WhatsApp kutoka kwenye programu ya WhatsApp Business.
- Fungua programu ya WhatsApp Business.
- Kwenye Android, gusa Chaguo zaidi, Kwenye iPhone, gusa Mipangilio.
- Gusa Zana za Biashara > Facebook na Instagram.
- Gusa akaunti yako ya Facebook iliyounganishwa > Ondoa WhatsApp > ONDOA.
- Mara baada ya kuondoa akaunti yako, haitaonekana tena kwenye skrini ya Facebook na Instagram.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- MFUMO wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) Online
- JINSI ya kupata mikopo ya vijana na wanawake
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
