LIVE MBEYA CITY VS YANGA Download HAPA kutazama LIVE kwenye Simu Yako Leo Saa 10:00 Jioni.

LIVE SIMBA VS POLISI TANZANIA Download HAPA kutazama LIVE kwenye Simu Yako Leo Saa 1:00 Usiku. 

KAMATI ya watu 14 yaundwa kutatua mgogoro wa Wafanyabiashara Kariakoo

Filed in Habari by on 18/05/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

KAMATI ya watu 14 yaundwa kutatua mgogoro wa Wafanyabiashara Kariakoo

KAMATI ya watu 14 yaundwa kutatua mgogoro wa Wafanyabiashara Kariakoo

KAMATI ya watu 14 yaundwa kutatua mgogoro wa Wafanyabiashara Kariakoo

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameunda tume ya watu 14 ambayo itachakata kero na mapendekezo ya Wafanyabiashara wa Soko la Kimataifa la Kariakoo.

Waziri Mkuu, Majaliwa ameunda tume hiyo May 17, 2023 alipozungumza na Wafanyabiashara wa Soko hilo katika viwanja vya Mnazi Mmoja vilivyopo Jijini Dar es Salaam.

Tume hiyo ambayo imepewa siku 14 kuja na mapedekezo ya kutatua changamoto za Wafanyabiashara, itakuwa na Watendaji saba kutoka Serikalini na saba kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara.

Kwa upande wa Serikali, Waziri Mkuu amewataja Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Katibu Mkuu

Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA, Kamishna wa Sera wa TRA.

Kwa Upande wa Wafanyabiashara ni Mwenyekiti wa Taifa wa Wafanyabiashara, Mwenyekiti wa wafanyabiashara Kariakoo, na Wafanyabiashara wengine ni Ismail Masoud Kutoka Tanga, Fred Ngajiro (Vunja Bei) Awadh Mpandira, Salome Mgaya (Mama Bonge), na Omari Hussein kutoka Zanzibar.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa amesema Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anathamini Sekta ya Biashara na ameagiza kufanya maboresho kuanzia Wafanyabiashara wadogo hadi wakubwa ili kukuza Sekta hiyo.

“Serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Rais wetu, itaendelea kuimarisha Biashara zenu, kilio chenu tumekisikia, na ndiyo maana nimerudi tena kwa maelekezo ya Rais wetu, naomba muone nia ya dhati ya Serikali yenu kwamba mfanye Biashara zenu na mpate mafanikio”.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza kamati aliyounda kufanya mapitio ya madai ya Wafanyabiashara ambao mizigo yao imekamatwa na kuwasilisha mapendekezo kwa Kamishna wa TRA ili waone uwezekano wa kuiachia kwa kutengeneza unafuu kwa wafanyabiashara.

“Kamishna wa TRA, mizigo imekaa sana na mingine imeshuka thamani, uking’ang’ania ulipwe kodi ile ile hutapata chochote itaharibika, kaangalie utaratibu mwingine nafuu.”

Akihitimisha mazungumzo na Wafanyabiashara hao, Mheshimiwa Majaliwa amewasihi Wafanyabiashara hao kuendelea na Biashara zao.

“Nawasihi mrudi kazini ili mkafanye Biashara, kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan naomba mridhie kufungua Maduka ili tunusuru soko la kimataifa liendelee kuwa na heshima yake.”

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *