Nijuze Habari

KARANI wa SENSA hajafika kwako? zimeongezwa siku 7 (fanya haya ili uesabiwe)

Filed in Habari by on 29/08/2022 0 Comments

KARANI wa SENSA hajafika kwako? zimeongezwa siku 7 (fanya haya ili uesabiwe)KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi Mhe. Anne Makinda akizungumza na Waandishi wa habari August 29,2022 wakati akitoa taarifa kuhusu maendeleo ya zoezi la SENSA ambalo lilitakiwa kuisha Leo.

Nijuze Habari Application

KARANI wa SENSA hajafika kwako? zimeongezwa siku 7 (fanya haya ili uesabiwe)

KARANI wa SENSA hajafika kwako? zimeongezwa siku 7 (fanya haya ili uesabiwe)KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi Mhe. Anne Makinda akizungumza na Waandishi wa habari August 29,2022 wakati akitoa taarifa kuhusu maendeleo ya zoezi la SENSA ambalo lilitakiwa kuisha Leo.

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Anne Makinda amesema asilimia 93.45 ya kaya zote Tanzania zimehesabiwa hadi kufikia Jumatatu August 29, 2022 saa 2 asubuhi na hivyo wameamua kuongeza muda wa ziada wa siku 7 kukamilisha zoezi hilo.KARANI wa SENSA hajafika kwako? zimeongezwa siku 7 (fanya haya ili uesabiwe)

“Zoezi la kuhesabu watu lililoanza usiku wa kuamkia tarehe August 23 2022 hadi kufikia August 29 2022 linaendelea vizuri ambapo kiwango cha kaya ambazo zimehesabiwa kimefikia asilimia 93.45. Haya ni mafanikio makubwa yaliyotokana na utayari mkubwa wa wananchi kushiriki kuhesabiwa kwa ajili ya maendeleo ya nchi” amesema Makinda.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kutoa taarifa hiyo Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Mhe. Anne Makinda amesema zoezi la kuhesabu watu linatarajiwa kukamilika hii Leo lakini kwa wananchi ambao bado hawajahesabiwa wafike katika ofisi za Serikali ya Mtaa au kupiga simu namba 0753-665491 au 0626-141515, 0784665404, 0656279424 kutoa taarifa zao kwa karani wa SENSA na atawafikia kuwa hesabu na zoezi hilo litadumu kwa siku saba kuanzia Agosti August 30 hadi September 05,2022.KARANI wa SENSA hajafika kwako? zimeongezwa siku 7 (fanya haya ili uesabiwe)

Ameongeza kuwa ifikapo August 30 hadi September 01,2022 kutakuwa na zoezi la SENSA ya majengo yote ikiwa ni pamoja na ofisi ili kuipa nafasi Serikali kuboresha sera yake ya makazi hivyo ametumia fursa hiyo amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani wa SENSA kwa kutoa taarifa sahihi.

“Wananchi ambao hajahesabiwa hakikisheni licha ya kuachiwa fomu za kujaza mtumie fursa hii kwa kupiga simu kwani waratubu na makarani wote wako kazini muhesabiwe ni kwa faida yenu na nchi kiujumla nafasi bado ipo”,amesema.KARANI wa SENSA hajafika kwako? zimeongezwa siku 7 (fanya haya ili uesabiwe)

Naye, Mkurugenzi wa Shughuli za Takwimu katika Ofisi za Taifa ya Takwimu Bi. Emilian Karugendo amesema makarani wa Vijijini ndiyo waliopewa Power Bank kwaajili ya Vishikwambi vyao kutokana na changamoto ya baadhi ya maeneo yao bado umeme haujafikiwa wanaofanya maeneo ya Mijini wao umeme upo kila mahali na tumekuwa tukiwapigia Tanesco kama kuna hitilafu ya umeme.

Ameongeza kuwa Vifaa vinavyotumika katika shughuli ya SENSA baada ya kazi hiyo vitatumika kwa mpango Maalumu wa kiserikali huku akiwatoa hofu Makarani wote kuwa watalipwa malipo yao baada ya kazi.

Makinda ametoa Muongozo kwa wananchi ambao watakuwa hawajahesabiwa mpaka kufikia jana jioni kuwa bado wana nafasi ya kuhesabiwa akitoa utaratibu ikiwemo kwenda kwenye ofisi za serikali za mitaa wanakoishi.

Mwananchi unashauriwa uende moja kwa moja kwenye ofisi za Serikali za mitaa na onana na Mwenyekiti au Mtendaji wa mtaa unaoishi na hakikisha unawachia namba ya mawasiliano ili karani akufuate ulipo na kuanza kazi ya kukuhesabu.

Kutokana na umuhimu wa kipekee wa SENSA, mshairi wa kisasa, Bw.Lwaga Mwambande anakushirikisha jambo muhimu ambalo litakuwezesha wewe ambaye bado haujahesabiwa uweze kuchangamkia fursa kwa manufaa yako na Taifa kwa jumla, karibu;

1.Ni bora utupigie, upate kuhesabiwa,
Na wala usisinzie, ukose kuhesabiwa,
Namba uziangalie hapa, piga upate fikiwa, Sensa kwaajili yetu, usikose hesabiwa.

2.Zoezi linaishia, hakikishs wahesabiwa, Tunakuhakikishia, na wewe utafikiwa, Popote pale sikia, ni haki kuhesabiwa,
Sensa kwaajili yetu, usikose hesabiwa.

3.Tumefikia pazuri, ni wengi wamefikiwa, Lakini tuna hadhari, pengine hujafikiwa, Usikae kusubiri, ita utahesabiwa, Sensa kwaajili yetu, usikose hesabiwa.

4.Heko kwa Watanzania, nyote mliofikiwa, Na wageni wenye nia, mlokwishahesabiwa,
Nyie mliosalia, tafadhali hesabiwa, Sensa kwaajili yetu, usikose hesabiwa.

5.Muhimu ukafikiwa, wala usijechelewa, Umuhimu waelewa, takwimu zinawaniwa, Mipango tukipangiwa, iwe tunayoelewa, Sensa kwaajili yetu, usikose hesabiwa.

6.Tuko mwishoni mwishoni, muhimu kuhesabiwa,
Wala usione soni, piga simu hesabiwa, Wako wengi Makarani, hakika utafikiwa,
SENSA kwaajili yetu, usikose hesabiwa.

7.Tupo tayari tayari, simu yako yasubiriwa, Ukipiga ni habari, Karani utatumiwa,
Takuhesabu vizuri, nasi tutafurahia, Sensa kwaajili yetu, usikose hesabiwa.

8.Mmesalia wachache, ni bado kuhesabiwa,
Tokeza usijifiche, takwimu zinawaniwa, Kupiga simu usiache, na wewe utafikiwa,
Sensa kwaajili yetu, usikose hesabiwa.

9.Asanteni ninyi nyote, mlokwisha hesabiwa,
Shukurani mzipate, kweli tumewaelewa, Kesho takwimu tupate, vema zipate tumiwa, Sensa kwaajili yetu, usikose hesabiwa.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.