Kassim Dewji ang’atuka Simba Sports Club

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


Kassim Dewji ang’atuka Simba Sports Club
Kassim Dewji ambaye ni Kiongozi Mwandamizi ndani ya Simba SC ametanga kustaafu ngazi zote za kuteuliwa au kuchaguliwa ndani ya Klabu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Msimbazi Jijini Dar es salaam Leo Jumatatu tarehe 6 February, 2023
Kassim Dewji alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, akirithi mikoba hiyo kutoka kwa Zacharia Hanspope aliyefariki Dunia.
Kassim Dewji amesema kuwa anatastaafu ngazi zote za uongozi ndani ya Simba kutokana na Majukumu ya Kibiashara na Kifamilia.
Dewji katika barua yake amesema kuwa ni wakati mwafaka yeye kama Mzee kupumzika katika nafasi za uendeshaji na maamuzi katika klabu hiyo Pendwa.
Kupitia barua yake kwenda Simba Sports Club Kassim Dewji ameandika;
“Nikiwa mwanachama na kiongozi mstaafu katika nafasi tofauti tofauti katika kipindi chote naomba kukujulisha kuwa kutokana na majukumu ya kibiashara na kifamilia nitastaafu ngazi zote za kuteuliwa au kuchaguliwa”
“Nimekuwa katika Familia ya Simba kwa muda mrefu toka mwaka 1989 nimefurahi Mafanikio mengi katika kipindi hicho nimefanikiwa kuwaandaa Viongozi mbalimbali katika nyadhifa tofauti kuiongoza Simba“
“Simba Spots Club ni Klabu kubwa na inachangamoto nyingi katika kipingi hiki inahitaji Vijana katika kuliongoza Jahazi hili”
“Ni wakati mwafaka sisi Wazee tupumzike katika nafasi za Uendeshaji na maamuzi katika klabu yetu Pendwa”
“Badala yake tubakie katika nafasi ya kushauri ikihitajika. Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru Wanachama na Wapenzi wote wa Simba Sports Club kwa Ushirikiano walionipa nikiwa katika Uongozi kwa miaka yote 25 pia nawashukuru wote walionipa Ushauri na kunikosoa pale walipoona nakwenda tofauti na maono yao”
“Hakika nimefurahia Maisha ndani ya Simba na nastaafu nikielewa ni muda mwafaka” amesema Kassim Dewji.
Kassim Dewji ni moja ya viongozi wenye alama kubwa ndani ya klabu ya Simba kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa akiwa katika nafasi mbalimbali.
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.