telegram Nijuze Habari

KILICHOJIRI Press Conference ya Simba SC, March 28,2022

Filed in Michezo by on 29/03/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

KILICHOJIRI Press Conference ya Simba SC, March 28,2022

Simba SC, Simba, Simba Sports Club, Msimbazi Dar es salaam, Simba SC vs US Gendarmerie Nationale, CAF Confederation Cup, Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Kombe la Shirikisho, RB Berkane, ASES Mimosas, Simba Nguvu Moja, Simba Tanzania, Simba SC Tanzania, Ligi Kuu Tanzania Bara, NBC Premier League, Union Sportive de la Gendarmerie Nationale, Stade Général Seyni Kountché, Union Sportive de la Gendarmerie Nationale is a Nigerien football club based in Niamey.

MENEJA wa habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amewataka mashabiki kuendelea kununua tiketi mapema ili kuhakikisha wanatumia nafasi zote 35,000 walizopewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya USGN ambao utapigwa Jumapili, April 03 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Ahmed amesema waliomba ongezeko la idadi ya mashabiki kupitia TFF lakini kutokana na changamoto ya covid, CAF wameshikilia msimamo wa mashabiki 35,000

“Tumeruhusiwa mashabiki 35,000. Awali tuliomba kuongeza idadi ya mashabiki kupitia kwa TFF lakini kwa sababu ya mambo ya Covid wameruhusu idadi ya mashabiki 35,000. Mashabiki ambao wanataka kuja kuona mchezo wanunue tiketi mapema”

“Wapinzani wetu USGN watawasili nchini alfajiri ya siku ya Alhamisi. Tumetoa taarifa hiyo kwa kujua wana wenyeji wao hapa nchini ili wakawapokee wageni wao”

“Tiketi tayari zinauzwa mitandaoni. Kwa mashabiki wetu waliopo mikoani hakuna haja ya kununua tiketi hadi wakifika Dar, huko huko wanaweza kununua kwa simu”

“Tiketi vituoni zitaanza kuuzwa kuanzia jumatano baada ya mchezo wa Taifa Stars. Safari hii nyimbo zetu zitapigwa kupitia spika za uwanja na watu wataitikia kwa pamoja, na tayari zimesharekodiwa kwenye mfumo rasmi,” alisema Ahmed

Akizungumzia maandalizi ya kikosi, Ahmed amesema timu tayari iko kambini, wachezaji wakiwa na morali kubwa kuelekea mchezo huo ambao wanahitaji kushinda

“Tunawashukuru TTF kwa kuwaruhusu wachezaji wetu waliokuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa kurejea kambini kujiandaa na mchezo wetu ujao. Kambi ilianza jana na mazoezi yalianza jana. Mwalimu amefurahi namna wachezaji wameanza mazoezi. Wachezaji wana morali ya hali ya juu na mwalimu anaamini watakuwa na mwendelezo huo kwenye mchezo wetu wa Aprili 3.”

“Tutaingia kwenye mchezo wa jumapili tukiwa na lengo moja tu, USHINDI. Tutaingia kwa nguvu moja, kwa ari ya juu na lengo ni moja tu ushindi. Niseme kwa nia ambayo tuko nayo robo fainali hii hapa.”

“Kwa sisi kama Simba tunaamini wachezaji hawatakuwa na pressure ya mchezo. Kwa kocha, ni kocha mkubwa tunajua ana uwezo wa kuivusha timu salama. Hatuna mashaka. Mpaka jana wanaingia kambini tulikuwa na majeruhi mmoja tu, Hassan Dilunga. Sadio Knaoute ambaye alikosekana kwenye mchezo uliopita jana alianza mazoezi”

“Tumeshajifunza kutokana na makosa yaliyopita, tunaenda kuwakabili USGN tukiwaheshimu na hatutarudia makosa ya awali. Mambo ya bonus yapo sawa. Huwa inatokea muda mwingine boss Mo anawaongezea lakini hata kabla ya ya mechi wachezaji wanajua kabisa kuwa bonus itakuwepo,” aliongeza Ahmed

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *