Nijuze Habari

KIPA Mcomoro atua Azam FC

Filed in Usajili by on 13/07/2022 0 Comments

Ali Ahamada Azam FCKLABU ya Azam FC imetangaza kukamilisha usajili wa kipa mkongwe wa kimataifa wa Comoro mzaliwa wa Ufaransa, Ali Ahamada kwa mkataba wa miaka mitatu.

Nijuze Habari Application

KIPA Mcomoro atua Azam FC

Ali Ahamada Azam FCKLABU ya Azam FC imetangaza kukamilisha usajili wa kipa mkongwe wa kimataifa wa Comoro mzaliwa wa Ufaransa, Ali Ahamada kwa mkataba wa miaka mitatu.

Ali Ahamada Azam FCAhamada, mwenye umri wa miaka 30, ni mmoja wa makipa wazoefu, aliyewahi kucheza klabu mbalimbali barani Ulaya, ikiwemo miamba ya Ufaransa, Toulouse, inayoshiriki Ligue 1 na Brann ya Norway.

Ahamada amesaini mkataba mbele ya mmiliki wa timu hiyo Yusuf Bakhresa na C.E.O Abdulkarim Amin.

Ali Ahamada Azam FCKabla ya hapo alicheza Toulouse kuanzia mwaka 2011 alikodaka jumla ya mechi 133 hadi anaondoka Ufaransa na kwenda Kayserispor ya Uturuki mwaka 2016 hadi 2019 alipohamia Kongsvinger ya Norway pia.

Toulouse alianza kuichezea timu ya vijana mwaka 2009 akitokea Martigues iliyomuibua mwaka 2000 na kumkuza kisoka.

Ali Ahamada Azam FCUbora wa Ahamada, ulimfanya kuchezea timu ya Taifa ya Ufaransa chini ya umri wa miaka 20, akiwa sambamba na mastaa wengine Varane, Coquelin, Lacazette na Kakuta.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.