KISINDA ruksa kukipiga Yanga SC

Filed in Usajili by on 15/09/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

KISINDA ruksa kukipiga Yanga SC

Tuisila Kisinda Yanga SC, Tuisila Kisinda arejea Yanga, Tuisila Kisinda arejea Young Africans, Tuisila Kisinda, Tuisila Kisinda Yanga, Kisinda Yanga SC, Kisinda arejea Yanga, TK Master arejea Yanga SC, TK Master arejea Young Africans.

 

KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitisha usajili wa Tuisila Kisinda kuichezea Klabu ya Yanga SC baada ya klabu hiyo kumuhamisha Mchezaji wake wa kigeni Lazarous Kambole.

Awali kamati hiyo ilizuia Usajili wa Kisinda licha ya kuwa ulifanyika ndani ya Dirisha la Usajili kwa vile tayari Yanga SC ilikuwa na wachezaji 12 wa kigeni.

Licha ya changamoto hiyo, pia Kisinda aliombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ambayo tayari imepatikana.

Hivyo kwa kumuhamisha kambole Yanga imepata nafasi ya kumsajili Kisinda kama ilivyokuwa imeshauriwa huko nyuma.

Kwa mujibu wa kanuni ya 62(1) ya Ligi Kuu Toleo la 2022, Klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12.

Taarifa hiyo kutoka TFF imesema kuwa Kambole amejiunga na timu ya Wakiso Giants inayocheza Ligi Kuu ya Uganda, na tayari TFF imetoa ITC.

Tuisila Kisinda Yanga SCYanga ilimrejesha Kisinda mwenye umri wa miaka 22 kutoka RS Berkane ya Morocco, iliyomsajili kutoka Yanga SC August 13,2021 pamoja na Clatous Chama wa Simba SC.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , , , , , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *