KITAYOSCE FC Tabora yapanda Ligi Kuu 2023/2024

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


KITAYOSCE FC Tabora yapanda Ligi Kuu 2023/2024

KITAYOSCE FC Tabora yapanda Ligi Kuu 2023/2024
TIMU ya Kitayosce FC imepanda daraja hadi Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2023/2024 baada ya Ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya African Sports ya Tanga, mchezo uliopigwa Jana May 13, 2023 Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
Baada ya Ushindi huo Kitayosce ilifikisha pointi 60 ikiwa pointi ni moja zaidi ya Pamba FC ya Mwanza ambayo pia ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Fountain Gate Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Kitayosce inaungana na JKT Tanzania FC ambao ni Mabingwa wa Championship waliomaliza kwa Ligi hiyo kwa 63 kupanda Ligi Kuu ya NBC 2023/2023?
Katika hatua nyingine, Pamba FC iliyomaliza nafasi ya 3 itacheza na Mashujaa FC iliyomaliza nafasi ya nne na mshindi wa jumla kwenye michezo miwili atacheza na timu iliyoshuka kutoka Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kuwania kupanda Ligi Kuu.
Play Off ya Ligi ya NBC itazikutanisha (home and away) timu zitakazomaliza nafasi za 13 na 14, na Mshindi wa jumla atabaki Ligi Kuu, anayeshindwa atashuka moja kwa moja na atakutana na Mshindi kati ya Pamba na Mashujaa kuwania kupanda Ligi Kuu ya NBC.
Gwambina na Ndanda FC zilizojitoa Ligi hiyo zimeshuka, wakati Copco, Green Warriors, Pan African na Africans Sports zitakwenda kwenye mchujo wa kuwania kubaki Championship.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- MFUMO wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) Online
- JINSI ya kupata mikopo ya vijana na wanawake
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.