Nijuze Habari

KOCHA mpya Simba atajwa

Filed in Usajili by on 21/06/2022 0 Comments

Tarik Sektioui Simba SCINAELEZWA kuwa mchakato wa kupitia wasifu wa kumpata Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba SC atakayerithi mikoba ya Pablo Franco, umekamilika na muda si mrefu atatangazwa kuchukua nafasi hiyo.

Nijuze Habari Application

KOCHA mpya Simba atajwa

Tarik Sektioui Simba SCINAELEZWA kuwa mchakato wa kupitia wasifu wa kumpata Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba SC atakayerithi mikoba ya Pablo Franco, umekamilika na muda si mrefu atatangazwa kuchukua nafasi hiyo.

Tarik Sektioui Simba SCHadi kufikia jana Jumatatu ya June 20,2022, kulikuwa na makocha wawili ambao walikuwa wakiangaliwa kwa mara ya mwisho ili kumpitisha mmoja akiwemo kocha wa zamani wa RS Berkane ya Morocco, Tarik Sektioui, Mwingine ni Jozef Vukušič raia wa Slovakia, lakini taarifa zinadai kuwa Sektioui ana nafasi kubwa ya kupewa mikoba hiyo.

Kocha huyo raia wa Morocco mwenye umri wa miaka 45, October 25, 2021 aliiongoza RS Berkane kutwaa Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF Confederation Cup) kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Pyramids FC ya Misri.

Tarik Sektioui Simba SCAidha imeelezwa kuwa baada kuchakata na kufanya mahojiano na makocha waliosalia kwenye ile orodha ya waliokuwa wakiwahitaji, Sektioui ameonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumrithi Pablo.

Kocha huyo alijiuzulu kuitumikia RS Berkane March 07, 2021 na nafasi yake ikachukuliwa na Kocha Juan Pedro Benali raia wa Hispania, alipoondoka akateuliwa Florent Ibenge ambaye yupo hadi sasa.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.