Nijuze Habari

Logo za GSM zaondolewa Taifa

Filed in Michezo by on 10/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application
HATIMAYE klabu ya Simba SC na Shirikisho la soka Tanzania TFF wamefikia makubaliano ya pamoja baada ya kuibuka utata kufuatia Simba SC kugomea logo ya kampuni ya GSM kutumika kwenye mkutano wake na wanahabari kuelekea mchezo wa watani wa jadi hapo kesho.
Logo hizo zilipambwa pia kwenye uwanja wa Mkapa utakaopigwa mchezo huo lakini baada ya mazungumzo hayo logo hizo sasa zimetolewa.
Aidha kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Simba SC wamechapisha ujumbe wa kuhamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo.

Kuelekea mchezo huo Kocha Mkuu wa Young Africans SC Nasreddine Al Nabi amesema kuwa; Derby ni kubwa na ngumu, timu zote mbili ni bora na amewaandaa wachezaji wake kuwa bora na kufuata mpango (plan) wa mechi kujua kile wanachotakiwa kukifanya.

Naye Kocha mwenyeji wa mchezo huo ambao utachezwa majira ya saa 11:00 jioni, Pablo Franco Martín amesema kuwa itakuwa mechi ngumu, timu itaenda kupambana kwaajili ya mashabiki wake na kuweza kupata pointi 3 za mchezo huo.

Awali, Klabu hiyo iliiandikia barua Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) kuhoji juu ya mkataba wa udhamini wa kampuni ya GSM katika Ligi Kuu huku pia wakiwa wadhamini wa wapinzani wao, Young Africans SC.

Katika barua hiyo iliyosainiwa na Mtendaji Mkuu wa Simba, klabu hiyo ilisema haifahamu kwa undani juu ya mkataba huo wao watanufaika vipi zaidi tu ya kufahamishwa kutumia nembo ya GSM kwenye tiketi na jezi zao wakati wa mechi zinazofuata za Ligi hiyo.

Lakini pia Simba ilisema GSM kuwa wadhamini wa Ligi Kuu wazi inaleta mgongano wa kimslahi kwa sababu ni wadhamini wa Young Africans pia klabu ambayo kwa pamoja na mdhamini wao lengo lao ni kutwaa Ubingwa Ligi kama wao Simba SC.

November 23, mwaka huu GSM iliingia mkataba wa Udhamini Mwenza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa dau la Sh. Bilioni 2.1 ikiwa ni mkataba wa miaka miwili.

telegram Nijuze Habari

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.