Nijuze Habari

MABADILIKO tarehe ya Uchaguzi Mkuu Yanga SC

Filed in Michezo by on 05/07/2022 0 Comments

Tarehe ya Uchaguzi Mkuu Yanga SCKAMATI ya Uchaguzi ya Yanga imeurudisha nyuma kwa siku moja Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo kutoka July 10 hadi 09,2022, ambapo uchaguzi huo utafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Nijuze Habari Application

MABADILIKO tarehe ya Uchaguzi Mkuu Yanga SC

Tarehe ya Uchaguzi Mkuu Yanga SCKAMATI ya Uchaguzi ya Yanga imeurudisha nyuma kwa siku moja Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo kutoka July 10 hadi 09,2022, ambapo uchaguzi huo utafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Mwenyekiti huyo amesema sababu za kurudisha nyuma uchaguzi huo ni kupisha sikukuu ya Eid El Haj.

Mchungahela amesema mabadiliko hayo yametokana na taarifa ya Baraza Kuu la Waislam (BAKWATA) kutangaza kuwa Sikukuu ya Eid Al Haji ni July 10,2022.

Kampeni za uchaguzi zimefunguliwa rasmi jana Jumatatu July 04 na zitafika tamati July 08,2022.

Tarehe ya Uchaguzi Mkuu Yanga SCMchungahela pia ametangaza kurejeshwa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi Mustapha Himba anayewania Ujumbe Kamati ya Utendaji baada ya kushinda rufaa yake.

Matawi ambayo hayakuwa yamekamilisha michakato ya uchaguzi yanapaswa kuwasilisha orodha ya wajumbe watano ambao watashiriki uchaguzi.

Matawi ambayo hayatawasilisha majina mapema, wajumbe wake hawataruhusiwa kupiga kura.

Tarehe ya Uchaguzi Mkuu Yanga SCKatika hatua nyingine, mwenyekiti wa Klabu hiyo anayemaliza muda wake Dk Mshindo Msolla amesisitiza mshikamano miongoni mwa Wanayanga ili kuhakikisha wanayalinda mafanikio waliyopata na kuongeza mafanikio zaidi.

Dk Msolla amesema baada ya mabadiliko ya Katiba ambayo yamewezesha mfumo mpya, hakuona sababu ya kuwania nafasi ya Urais kwani yeye ni muumini wa utawala boram

Tarehe ya Uchaguzi Mkuu Yanga SCAidha Dk Msolla amesema amejiridhisha na uwezo wa wagombea waliojitokeza, wanaweza kuifikisha Yanga kule ambako kila mmoja anatamani.

Dk Msolla amesema hajaondoka Yanga kwa ubaya, bali ametimiza ahadi aliyotoa wakati akiwania Uwenyekiti wa klabu ya Yangam

“Sikuona sababu ya kurudisha fomu baadhi ya kujiridhisha kuwa wagombea waliojitokeza wanatosha”

“Kwa wale mnaokumbuka wakati wa kampeni nikiwa nawania Uwenyekiti, nilisema kama nitafanikiwa suala la Mabadiliko, ndani ya mwaka mmoja au miwili nitaachia madaraka kwa kuwa najua nitakuwa nimeipeleka klabu yangu katika sehemu sahihi,” alisema Dk Msolla

Dk Msolla amewaasa wagombea kutochafuana wakati wa kampeni, wahakikishe wanavunja makundi baada ya uchaguzi

“Nawaasa wagombea, hakuna sababu ya kuchafuana wakati wa kampeni, Nalisema hili kutokana na uzoefu wangu, wakati nikiwa nagombea lnilichafuliwa sana, hakuna sababu ya kufanya hivyo”

“Baada ya uchaguzi tuhakikishe tunaendelea kuwa wamoja kwa kuvunja makundi yetu. Ni umoja wetu ndio utakaofanya klabu yetu iweze kusonga mbele”

UNAWEZA PIA KUSOMA PIA👇

DOWNLOAD APP MPYA YA NIJUZE HABARI BURE HAPA

UPATE KUTAZAMA MECHI LIVE, MAGAZETI YA KILA SIKU ASUBUHI PAMOJA NA HABARI NYINGINE NYINGI.

TEMBEA NA DUNIA MKONONI MWAKO UKIWA NA APP HII, FURAHIA HABARI NA MATUKIO KILA WAKATI.

Download Bure App mpya ya Nijuze Habari kuweza kuangalia Mpira na utaweza kuona matokeo na ratiba ligi zote kubwa Duniani.

APP HII PIA INAKUSOGEZEA

👉Habari za Kitaifa na kimataifa kutoka vyanzo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania
👉Habari za Michezo na Usajili ndani na nje ya Tanzania
👉Breaking News
👉Elimu na Afya
👉Kutazama Mechi Mubashara za ndani na nje ya Tanzania
👉Taarifa ya Habari kila siku na Vipindi Mbalimbali kutoka Local Tvs
👉Kusikiliza Radio Online
👉Kucheck Movie kutoka (Maisha Magic Bongo na Maisha Magic East n.k)
👉Audio na Videos mpya kila siku
👉 Ajira mpya kila siku
👉Gospel na Makala mbalimbali.

BOFYA 👉👉👉 HAPA KUDOWNLOAD BURE

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.