Nijuze Habari

MABADILIKO ya muda, Simba vs Yanga ngao ya Jamii 2022, Viingilio vyawekwa wazi

Filed in Michezo by on 10/08/2022 1 Comment

MABADILIKO ya muda, Simba vs Yanga ngao ya Jamii 2022, Viingilio vyawekwa waziMCHEZO wa Ngao ya Jamii wa kuashiria Ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League 2022/2023) kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC unatarajiwa kupigwa Jumamosi hii ya August 13,2022 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini.

Nijuze Habari Application

MABADILIKO ya muda, Simba vs Yanga ngao ya Jamii 2022, Viingilio vyawekwa wazi

MABADILIKO ya muda, Simba vs Yanga ngao ya Jamii 2022, Viingilio vyawekwa waziMCHEZO wa Ngao ya Jamii wa kuashiria Ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League 2022/2023) kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC unatarajiwa kupigwa Jumamosi hii ya August 13,2022 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini.

Mchezo huo maarufu kama Debry ya Kariakoo umebadilishwa muda kutoka sasa 11:00 jioni na sasa utapigwa kuanzia saa 1:00 usiku siku hiyo hiyo Jumamosi August 13,2022.

Simba na Yanga zinakutana kwa mara ya kwanza msimu huu August 13,2022 kwenye mchezo huo wa ufunguzi wa Ligi Kuu, ambapo zitakutana tena October 23,2022 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League 2022/2023/

Shirikisho la Soka Tanzania TFF limetaja Viingilio vya mchezo huo kuwa ni Tsh 30,000 kwa VIP A, Tsh 20,000 kwa VIP B, huku VIP C ikiwa ni Tsh 15,000.

Viti vya rangi ya Machungwa itakuwa Tsh 7,000 na Viti vya Bluu pamoja na vya Kijani itakuwa Tsh 5,000.

Nijuze Habari itakuletea Mubashara Mchezo huo na Michezo mingine yote ya Ligi Kuu kupitia Nijuze Habari App, ambapo inapatikana Playstore pia unaweza Download HAPA.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: ,

About the Author ()

Comments (1)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Nkunzimana says:

    Ngoja tuone alieenda misri,mwingine kigamboni

Leave a Reply

Your email address will not be published.