telegram Nijuze Habari

Mabadiliko ya ratiba NBC Premier League

Filed in New by on 12/01/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPBL) imefanya mabadiliko machache kwenye ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) yakiathiri tarehe za michezo (12) muda wa kuanza kwa michezo sita (6) na kuipangia tarehe michezo mitatu (3) ambayo haikuwa na tarehe kwenye ratiba ya awali pamoja na mchezo wa kiporo kati ya Kagera Sugar FC dhidi ya Simba SC.

Mabadiliko hayo yamelenga kuepuka uwepo wa michezo ya viporo kutokana na ushiriki wa Simba SC kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF Confederation Cup), huku michezo mitatu (3) ikipangiwa tarehe baada ya kufahamika kwa hatma ya ushiriki wa klabu nnne ambazo ni Young Africans SC, Simba SC, Azam FC na Namungo FC kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Visiwani Zanzibar.

Aidha ratiba ya awali ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) ilizingatia ushiriki Klabu nne yaani Simba SC, Young Africans SC, Azam FC na Biashara United FC kwenye Michuano ya CAF kwa kuzipa nafasi ya kutosha kwaajili ya maandalizi ya safari na kucheza michezo ya michuano hiyo nyumbani na ugenini.

Kuondolewa kwa Klabu za Young Africans SC, Azam FC na Biashara United FC kwenye michuano ya CAF kumeilazimu Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPBL) kupitia upya ratiba ya Ligi Kuu na kufanya mabadiliko yafuatayo Ili Ligi iendelee kuchezwa bila kuwa na mechi za viporo kwa timu yoyote ikiwemo Klabu ya Simba SC ambayo inaendelea na mashindano hayo.

Hii ndiyo ratiba mpya baada ya mabadiliko hayo;

➡️January 16,2022
16:00 Coastal Union FC vs Young Africans SC

➡️January 17,2022
14:00 Polisi Tanzania FC vs Namungo FC
16:00 Mbeya City FC vs Simba SC

➡️January 18,2022
16:00 Mbeya Kwanza FC vs Azam FC

➡️January 26,2022
18:15 Kagera Sugar FC vs Simba SC

➡️February 03,2022
16:00 Ruvu Shooting FC vs Mbeya Kwanza FC
19:00 Simba SC vs Tanzania Prisons FC

➡️February 06,2022
19:00 Simba SC vs Mbeya Kwanza FC

➡️February 22,2022
16:00 Biashara United FC vs Azam FC

➡️February 27,2022
19:00 Young Africans SC vs Kagera Sugar FC

➡️March 01,2022
19:00 Azam FC vs Coastal Union FC

➡️March 03,2022
19:00 Simba SC vs Biashara United FC

➡️March 04,2022
19:00 Kagera Sugar FC vs Namungo FC

➡️March 05,2022
19:00 Azam FC vs Polisi Tanzania FC

➡️March 07,2022
19:00 Simba SC vs Dodoma Jiji FC

➡️March 27,2022
16:00 Polisi Tanzania FC vs Simba SC

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *