MABADILIKO ya Ratiba Yanga vs Singida BS, Azam vs Simba (Nusu Fainali ASFC 2023)

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


MABADILIKO ya Ratiba Yanga vs Singida BS, Azam vs Simba (Nusu Fainali ASFC 2023)

MABADILIKO ya Ratiba Yanga vs Singida BS, Azam vs Simba (Nusu Fainali ASFC 2023)
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesogeza mbele mchezo namba 096 wa hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) kati ya Singida BS dhidi ya Young Africans uliopangwa kuchezwa Mei 7, 2023 katika uwanja wa Liti, Singida mpaka hapo utakapopangiwa tarehe nyingine.
Mabadiliko hayo yametokana na maombi ya klabu ya Young Africans kupitia barua Kumb. Na. YASC/TFF/2023/120 kuomba kupata muda zaidi wa maandalizi ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini utakaochezwa Mei 10, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
TFF kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi imekubali kusogeza mbele mchezo wa Nusu Fainali ya ASFC na utapangiwa tarehe nyingine.
Katika hatua nyingine, TFF imeusogeza mbele kwa siku moja mchezo namba 095 wa hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) kati ya Azam FC dhidi ya Simba SC uliopangwa kuchezwa Jumamosi ya May 06, 2023 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara hadi Jumapili May 7, 2023.
TFF imesema kuwa mabadiliko hayo yamefanyika ili kutoa nafasi kwa timu za Azam FC na Simba kupata muda zaidi wa maandalizi kuelekea katika mchezo huo
Uongozi wa Yanga SC Jana Kupitia kwa rais wake Hersi Said uliliandika barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuomba moja kati ya mechi zake mbili wiki hii ifutwe ili wapate muda kidogo wa kujiandaa na mechi dhidi ya Marumo Gallants utakaochezwa May 10,2023.
DOWNLOAD VIDEO RAIS WA YANGA HERSI SAID AKITUMA MAOMBI TFF
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- MFUMO wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) Online
- JINSI ya kupata mikopo ya vijana na wanawake
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: Azam vs Simba (Nusu Fainali ASFC 2023), MABADILIKO ya Ratiba Yanga vs Singida BS