Nijuze Habari

MAKI anajitengenezea bomu mwenyewe

Filed in Michezo by on 19/08/2022 0 Comments

Na Yossima Sitta

Nijuze Habari Application

MAKI anajitengenezea bomu mwenyewe

Na Yossima Sitta

MAKI anajitengenezea bomu mwenyeweKITENDOcha Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Zoran Maki kuanza kuwakataa baadhi ya wachezaji wapya wa Simba kumeanza kuleta maswali mengi kwa mashabiki wa klabu hiyo wengine wamefikia hatua ya kuhoji uwezo wa kocha huyo.

Yaweza kuwa Maki yupo sahihi asilimia 100 kwa upande wake ila hatakuwa sahihi kwa asilimia 100 kwa utamaduni wa vilabu vyetu hasa Simba na Yanga kwani kuna baadhi ya wachezaji amewakataa anaweza kuondoka yeye na hao wachezaji wakabaki.

Kocha Maki anaweza akawa sahihi kwa kuwakataa Victor Akpar na Nassor Kapama kwa kusema hawapo kwenye mipango yake na hawafiti kwenye mfumo wake ila anaweza asiwe sahihi kwa wachezaji kama Moses Phiri, John Bocco, Nelson Okwa, Jonas Mkude na Clatous Chama.

Majina kama Chama, Phiri, Okwa na Mkude yanaweza kumfukuzisha kazi mara moja akiendelea na Msimamo wake unaosemwa kwa hao wachezaji. Maki akiwa pre-season Misri alisema hapendezwi na uchezaji wa Chama anacheza taratibu sana.

Pia kocha Maki alimwambia Nahodha wa Simba Bocco kuchagua mawili kuondoka au kubaki, alikataa usajili wa Moses Phiri na Nelson Okwa ndipo uongozi wa klabu hiyo ukamkatalia kata kata kwa kusema umetumia gharama kubwa kuwasajili wachezaji hao.

Kitendo cha kumpanga Jonas Mkude namba 8 na kumpa majukumu mengi ni kumtafutia sababu ya kumuacha kwenye mfumo wake. kocha Maki naona kabsa anamtafutia sababu Mkude ya kukaa bechi na ameuomba uongozi wa klabu hiyo kufanya usajili wa kiungo mkabaji haraka iwezekanavyo.

Kocha anajitegenezea bomu mwenyewe huwezi kuuaminisha umma kuwa Dejan Georgijević na Kyombo ni bora kuwazidi Phiri na Bocco au Mwenda ni bora kuliko Kapombe.

Anaweza akawa sahihi kwa Akpar na Kapama mashabaki na viongozi wakamuelewa ila sio kwa Chama na Phiri.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.