Nijuze Habari

MAKINDA afafanua jinsi watu watakavyohesabiwa siku ya SENSA 2022

Filed in Habari by on 18/08/2022 0 Comments

MAKINDA afafanua jinsi watu watakavyohesabiwa siku ya SENSA 2022KAMISAA wa Sensa, Anne Makinda, amebainisha namna watu watakavyohesabiwa wakati wa SENSA ya Watu na Makazi itakayofanyika August 23, 2022.

Nijuze Habari Application

MAKINDA afafanua jinsi watu watakavyohesabiwa siku ya SENSA 2022

MAKINDA afafanua jinsi watu watakavyohesabiwa siku ya SENSA 2022KAMISAA wa Sensa, Anne Makinda, amebainisha namna watu watakavyohesabiwa wakati wa SENSA ya Watu na Makazi itakayofanyika August 23, 2022.

Pamoja na kubainisha hayo, amesema kwamba SENSA hiyo itafanyika kwa siku sita huku akifafanua kuwa hakutakuwa na mapumziko wakati huo.

Akizungumza jana, SENSA hiyo itakavyokuwa, Makinda alisema kazi hiyo itafanyika kuanzia August 23 saa 6:01 usiku na kwamba itaendelea hadi muda wa siku sita, na akaongeza kuwa watakaokuwa safarini watapewa vitambulisho maalum ili wasihesabiwe mara mbili.

“Kuna makarani ambao wamepangiwa katika maeneo maalumu hususani wanaosafiri usiku kuanzia saa 6:01 usiku wa kuamkia siku ya sensa, tayari watakuwa katika maeneo hayo na watawauliza maswali machache tu na kisha kuwapatia vitambulisho, ili huko wanakokwenda wasihesabiwe tena,” alisema Makinda.

“Kazi hii haiwezi kuisha kwa siku moja, tumeweka muda hadi siku sita, ili kuhakikisha kazi hii inafanyika kwa ufasaha.

“Kila karani atakuwa na kiongozi katika eneo lake alilopangiwa, ambaye ni msimamizi wa maudhui, kwa hiyo atapanga ratiba aanzie mitaa ipi kwa siku hiyo ya kuamkia siku yenyewe ya SENSA hadi kumaliza katika muda ambao umepangwa, alisema.

Makinda alisema taarifa za msingi karani anatakiwa kupata anapofika ni idadi ya watu walioamkia Agosti 23 kwenye kila kaya.

“Kwa hiyo hata ikiwezekana ni vema siku ya SENSA kila kiongozi wa kaya akaandika idadi ya watu wake walioamkia siku hiyo ya SENSA kwenye kaya yake, ili kuepusha kusahau kwa sababu huenda karani asimfikie siku hiyo, alisema Makinda.

Maeneo mengine ambayo alisema ni maalum ambayo wataanza kuhesabu makarani kuanzia saa 6:01 ni hospitalini, viwanja vya ndege na Bandarini.

Pia alisema kwa kundi la watoto wa mitaani nako kuna makarani ambao wamepangwa kwaajili ya kazi hiyo.

“Yaani SENSA hii itapita kwenye maeneo yote, hakuna litakaloachwa, hata vijiweni huko nako watafikiwa. Na katika yale maeneo ambayo ni hatarishi tumepanga makarani wa kiume,” alibainisha.

Kuhusu maeneo ya jeshi, Makinda alisema huko watafanya wenyewe na watapewa mafunzo kama inavyofanyika kwa makarani wengine.

“Kwenye maeneo ya jeshi raia hawaingii, watafanya wenyewe huko isipokuwa watapewa mafunzo kama makarani wengine kwaajili ya kazi hizo, kwa hiyo hata kwa wafungwa gerezani watafanya wenyewe huko,”alisema Makinda.

Alisema makarani waliopewa mafunzo kwaajili ya kazi hiyo watakula kiapo cha kutunza siri na kwamba endapo atakuwapo atakayevunja kiapo hicho na kutoa siri atachukulia hatua ikiwamo kifungo cha miaka miwili au faini.

Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania, alisema baadhi ya maswali yatakayoulizwa siku ya SENSA kwa kaya ni pamoja na idadi ya wanakaya, Elimu yao, kama kuna wenye ulemavu na ni wa aina gani na shughuli wanazofanya

“Na huenda karani akataka kuona kitambulisho chochote ulichonacho iwe ni cha udereva, uraia, cheti cha kuzaliwa au kama una namba ya NIDA.

“Na hapa nataka wananchi waelewe kuwa si kwamba hawatohesabiwa wasipokuwa na hivyo vitambulisho, lengo ni kutaka kujua idadi ya wananchi wenye vitambulisho vya taifa ili tunapoishauri serikali tuseme ni asilimia ngapi wana vitambulisho.

Na katika hili naomba pia ikiwezekana waviandae kabisa, ili karani akifika wanamwonyesha tu na si kwenda kutafuta maana inaweza kupoteza muda,” alisisitiza.

telegram Nijuze Habari

Tags: , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.