Nijuze Habari

MAMBO muhimu Mwanachama wa Yanga unayopaswa kuyafahamu kuhusu Uchaguzi Mkuu

Filed in Michezo by on 06/06/2022 0 Comments

MAMBO muhimu Mwanachama wa Yanga unayopaswa kuyafahamu kuhusu Uchaguzi Mkuu.Kuelekea Uchaguzi wa Young Africans ambao unapaswa kufanyika July 10,2022, haya ni mambo manne muhimu ambayo Mwanachama wa Young Africans unapaswa kuyafahamu.

Nijuze Habari Application

MAMBO muhimu Mwanachama wa Yanga unayopaswa kuyafahamu kuhusu Uchaguzi Mkuu.

MAMBO muhimu Mwanachama wa Yanga unayopaswa kuyafahamu kuhusu Uchaguzi Mkuu.Kuelekea Uchaguzi wa Young Africans ambao unapaswa kufanyika July 10,2022, haya ni mambo manne muhimu ambayo Mwanachama wa Young Africans unapaswa kuyafahamu.

1:Nafasi zinazoshindaniwa ni saba (7), ambazo ni Rais, Makamu Rais na Wajumbe watano (5).

2:Fomu zinapatikana Makao Makuu ya Klabu mtaa wa Jangwani kwa ada ya Tsh. 200,000/= kwa nafasi ya Rais na Makamu Rais, na Tsh. 100,000/= kwa nafasi za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

3:Malipo yote yafanyike kupitia Benki katika akaunti ifuatayo; Jina la Benki: CRDB Jina la Akaunti: YANGA COLLECTION Nambari ya Akaunti: 0150419775800

Na pindi mgombea anapokwenda kuchukua fomu anakuja na risiti ya Benki ya malipo kwa nafasi anayogombea ndipo atapewa fomu.

Pia mgombea anapokuja kuchukua fomu lazima aje na Kadi ya Uanachama au kama bado hajapata kadi aje na ujumbe wa kulipia ada uliotumwa kwenye simu yake baada ya kulipia ada.

4:Fomu zitatolewa na kurejeshwa muda wa kazi kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 10:30 jioni (Jumatatu – Ijumaa).

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.