Nijuze Habari

MANARA aipinga hukumu ya TFF, apeleka Malalamiko Baraza la Michezo

Filed in Michezo by on 25/07/2022 0 Comments

Haji Sunday Manara Yanga SCHATIMAYE Msemaji wa Klabu ya Young Africans SC, Haji Manara ameweka wazi yaliyotokea kati yake na Rais wa TFF Wallace Karia, wakati wa mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ uliopigwa July 02,2022 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Nijuze Habari Application

MANARA aipinga hukumu ya TFF, apeleka Malalamiko Baraza la Michezo

Haji Sunday Manara Yanga SCHATIMAYE Msemaji wa Klabu ya Young Africans SC, Haji Manara ameweka wazi yaliyotokea kati yake na Rais wa TFF Wallace Karia, wakati wa mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ uliopigwa July 02,2022 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Jumatano ya July 21,2022 Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ ilitangaza kumfungia Haji Manara kwa miaka miwili na kumtoza faini ya Shilingi Milioni 20 kwa kwa kosa la kumtolea maneno yasiyofaa Rais wa TFF, Wallace Karia.

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari Serena Hotel mapema leo, Manara amesema anapinga hukumu hiyo kwa kuwa kanuni zilizotumika hazikusajiliwa na BMT.

Manara ameongeza kuwa mazingira ya tukio lililotokea kati yake na Rais Karia, akidai yaliyozungumzwa hayakua sahihi dhidi yake hadi kufungiwa kwa muda wa miaka miwili.

Manara amesema: Wakati wa half time ya Fainali ya (ASFC) nilikuwa nikiongea na Mkuu wa Mkoa wa Arusha maana nilikuwa najiandaa kuondoka Pressure ya mpira ilkuwa kubwa, wakati tunaendelea kuongea hatujamaliza hata dakika moja na pale kulikuwa na viongozi wengi, ghafla bila kutarajia wala sikujua imetoka wapi Rais wa TFF kwa ukali na makelele mengi alinifuata akaniambia wewe toka hapo, ondoka hapo.

Haji Sunday Manara Yanga SC“Nilikuwa naongea na Mkuu wa mkoa wakati ananinyooshea kidole na kunipgia makelee anawaangalia viongozi wa Coastal Union, nikamwambia nimefanya nini, akaniambia nimekwanbia ondoka ujue hapa kafa mtu, nikamwambia why kila siku unakuwa hivi, kwanini unapenda kufoka, Mkuu wa mkoa na viongozi wakanitoa nikaondoka.

“Baadaye akawa ananifuata nilipo akawa ananiambia nimekwambia hapa ondoka mimi ndiyo rais wa mpira, nikamwambia hiki unachokifanya sicho, imekuwa ni desturi, hunifanyii hivi kwa mara ya kwanza huoni heshima yangu unaishusha?,” amesema Msemaji wa Yanga, Haji Manara.

Aidha Manara amesema hukumu hiyo ililenga kumdhalilisha na kumzuia asishiriki Tamasha la Wiki ya Mwananchi ambalo kilele chake ni August 06,2022.

Manara amesema ameshindwa kukata rufaa kwa kuwa mpaka leo hajapewa nakala ya hukumu, ambayo Kamati ya Maadili ilitangaza kuwa ipo kwa anayeihitaji.

Anaamini anacheleweshwa kupata hukumu hiyo ili kuhakikisha wiki ya Mwananchi inapita pamoja na mchezo wa Ngao ya Jamii ili asifanye uhamasishaji.

“Hukumu hii pamoja na hukumu zote zilizotolewa na Kamati ya Maadili kwa kutumia kanuni ambazo hazijasaliwa na Baraza la Michezo (BMT) kama sheria za nchi zinavyoelekeza ni BATILI. Nimepeleka malalamiko BMT nikipinga hukumu hii ambayo haijafuata Sheria za nchi”

“Lakini pia hukumu hii ni uonevu mkubwa kwangu na imelenga kunidhalilisha na kunizuia nisishiriki Wiki ya Mwananchi na klabu ya Yanga. Hakuna matusi ambayo nilimtamkia rais Karia, pale jukwaa kulikuwa na Kamanda wa Polisi, Mkuu wa mkoa wa Arusha, Wakuu wa Wilaya, wabunge na viongozi wengine wa Serikali katika ngazi mbalimbali kama ningefanya makosa hayo naamini wasingeniacha”

“Rais Karia alinifokea pasipo sababu yoyote wakati nikizungumza na Mkuu wa mkoa na hii sio mara ya kwanza kunidhalilisha mbele za watu”

“Siku ile baada ya mchezo, Karia alitamka maneno mabaya ya kuidhalilisha Yanga ambayo kinywa changu hakiwezi kuyatamka. Maneno haya aliyasikia kila mmoja aliyekuwa pale jukwaani (VIP) na ushahidi wake upo,” alisema Manara

“Kamati ilininyiwa hata nafasi ya kujitetea kwa kuwa walikataa taarifa halali ya Hospitali ya Temeke ikithibitisha mimi kushindwa kuhudhuria shauri hilo kwa sababu nilikuwa mgonjwa,” ameongeza Manara

Manara ameendelea na kuongeza kuwa “Licha ya kuwa mimi ndio niliyetolewa maneno na Rais Karia ila Ras alisema niende kwake nikaenda na Eng Hersi na akaniambia niombe msamaha mbele ya vyombo vya habari nikaomba nikijua jambo limeisha lakini siku ya pili nikaletewa barua kuitwa kamati ya maadili

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.