Nijuze Habari

MANULA bado yupo sana Simba SC

Filed in Usajili by on 20/07/2022 0 Comments

 

Nijuze Habari Application

 

MANULA bado yupo sana Simba SC

Aishi Manula Simba SCUongozi wa Klabu ya Simba SC, umethibitisha kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba mpya wa miaka mitatu mlinda mlango nambari moja Tanzania Aishi Salum Manula.

Taarifa za kumuongeza mkataba Mlinda Lango huyo zimetolewa leo Jumatano July 20, 2022, kupitia Simba APP pamoja na Kurasa za Mitandao ya Kijamii za Klabu hiyo.

Akiwa na Simba SC Manula amefanikiwa kuchukua mataji manne ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho ASFC’ mara mbili na kuwa sehemu ya kikosi kilichotinga hatua ya Robo Fainali Afrika mara tatu ngazi ya Vilabu.

Manula ambaye amekuwa kwenye kiwango kizuri kwa zaidi ya miaka minne akiwa na Simba SC sasa ataendelea kuwepo kwa wanalunyasi hao hadi mwaka 2025.

Kwa sasa Manula yupo kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars’ akijiandaa na mchezo wa kuwania Kufuzu Fainali za Mataifa Bingwa Afrika ‘CHAN’ dhidi ya Somalia.

Mchezo ambao utapigwa Jumamosi hii ya July 23, 2022 kwenye dimba la Benjamin Mkapa kuanzia saa 10:00 jioni na kukufikia LIVE kupitia App yetu ya Nijuze Habari.

telegram Nijuze Habari

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.