Nijuze Habari

MASWALI yote yatakayoulizwa siku ya SENSA ya Watu na Makazi 2022

Filed in Habari by on 22/08/2022 0 Comments

OFISI ya Taifa ya Takwimui (NBS) inaendelea na maandalizi ya Sensa ya watu na makazi ya itakayofanyika August, 2022 nchini Tanzania.MASWALI 12 yatakayoulizwa siku ya SENSA ya Watu na Makazi 2022

Nijuze Habari Application

MASWALI yote yatakayoulizwa siku ya SENSA ya Watu na Makazi 2022.

OFISI ya Taifa ya Takwimui (NBS) inaendelea na maandalizi ya Sensa ya watu na makazi ya itakayofanyika August, 2022 nchini Tanzania.MASWALI 12 yatakayoulizwa siku ya SENSA ya Watu na Makazi 2022

SENSA hiyo inatarajiwa kuwa tofauti na zilizopita kwani itahusisha masuala tofauti ikiwemo matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika ukusanyaji wa taarifa, lakini pia itakusanya taarifa za Makazi.

Sensa ya mwaka 2022 itakuwa ni SENSA ya sita kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

SENSA nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.

Ili kufanikisha hilo, watu wote wanaokuwepo nchini siku ya SENSA wataulizwa maswali kuanzia 12 ambayo ni;

1:Taarifa za kidemografia (umri, jinsi, uhusiano, hali ya ndoa, uraia, n.k.

2:Maswali yanayohusu ulemavu.

3:Taarifa za Elimu.

4:Maswali ya uhamaji pamoja na taarifa za Watanzania wanaoishi nje ya nchi.

5:Maswali kuhusu umiliki wa nyaraka za kitaifa (vitambulisho vya NIDA, Mzanzibari mkazi, cheti cha kuzaliwa, hati ya kusafiria, na leseni ya udereva).

6:Shughuli za kiuchumi.

7:Umiliki wa ardhi na taarifa za TEHAMA.

8:Taarifa za Uzazi na Vifo vilivyotokea ndani ya kaya.

9:Vifo vitokanavyo na uzazi.

10:Hali ya nyumba za kuishi na umiliki wa rasilimali mbalimbali.

11:Maswali ya kilimo na mifugo.

12:Mifuko ya hifadhi ya jamii.

👉SOMA ZAIDI HAPA CHINI👇👇👇👇

MAKINDA afafanua jinsi watu watakavyohesabiwa siku ya SENSA 2022

MAKINDA afafanua jinsi watu watakavyohesabiwa siku ya SENSA 2022KAMISAA wa Sensa, Anne Makinda, amebainisha namna watu watakavyohesabiwa wakati wa SENSA ya Watu na Makazi itakayofanyika August 23, 2022.

Pamoja na kubainisha hayo, amesema kwamba SENSA hiyo itafanyika kwa siku sita huku akifafanua kuwa hakutakuwa na mapumziko wakati huo.

Akizungumza jana, SENSA hiyo itakavyokuwa, Makinda alisema kazi hiyo itafanyika kuanzia August 23 saa 6:01 usiku na kwamba itaendelea hadi muda wa siku sita, na akaongeza kuwa watakaokuwa safarini watapewa vitambulisho maalum ili wasihesabiwe mara mbili.

“Kuna makarani ambao wamepangiwa katika maeneo maalumu hususani wanaosafiri usiku kuanzia saa 6:01 usiku wa kuamkia siku ya sensa, tayari watakuwa katika maeneo hayo na watawauliza maswali machache tu na kisha kuwapatia vitambulisho, ili huko wanakokwenda wasihesabiwe tena,” alisema Makinda.

“Kazi hii haiwezi kuisha kwa siku moja, tumeweka muda hadi siku sita, ili kuhakikisha kazi hii inafanyika kwa ufasaha.

“Kila karani atakuwa na kiongozi katika eneo lake alilopangiwa, ambaye ni msimamizi wa maudhui, kwa hiyo atapanga ratiba aanzie mitaa ipi kwa siku hiyo ya kuamkia siku yenyewe ya SENSA hadi kumaliza katika muda ambao umepangwa, alisema.

Makinda alisema taarifa za msingi karani anatakiwa kupata anapofika ni idadi ya watu walioamkia Agosti 23 kwenye kila kaya.

“Kwa hiyo hata ikiwezekana ni vema siku ya SENSA kila kiongozi wa kaya akaandika idadi ya watu wake walioamkia siku hiyo ya SENSA kwenye kaya yake, ili kuepusha kusahau kwa sababu huenda karani asimfikie siku hiyo, alisema Makinda.

Maeneo mengine ambayo alisema ni maalum ambayo wataanza kuhesabu makarani kuanzia saa 6:01 ni hospitalini, viwanja vya ndege na Bandarini.

Pia alisema kwa kundi la watoto wa mitaani nako kuna makarani ambao wamepangwa kwaajili ya kazi hiyo.

“Yaani SENSA hii itapita kwenye maeneo yote, hakuna litakaloachwa, hata vijiweni huko nako watafikiwa. Na katika yale maeneo ambayo ni hatarishi tumepanga makarani wa kiume,” alibainisha.

Kuhusu maeneo ya jeshi, Makinda alisema huko watafanya wenyewe na watapewa mafunzo kama inavyofanyika kwa makarani wengine.

“Kwenye maeneo ya jeshi raia hawaingii, watafanya wenyewe huko isipokuwa watapewa mafunzo kama makarani wengine kwaajili ya kazi hizo, kwa hiyo hata kwa wafungwa gerezani watafanya wenyewe huko,”alisema Makinda.

Alisema makarani waliopewa mafunzo kwaajili ya kazi hiyo watakula kiapo cha kutunza siri na kwamba endapo atakuwapo atakayevunja kiapo hicho na kutoa siri atachukulia hatua ikiwamo kifungo cha miaka miwili au faini.

Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania, alisema baadhi ya maswali yatakayoulizwa siku ya SENSA kwa kaya ni pamoja na idadi ya wanakaya, Elimu yao, kama kuna wenye ulemavu na ni wa aina gani na shughuli wanazofanya

“Na huenda karani akataka kuona kitambulisho chochote ulichonacho iwe ni cha udereva, uraia, cheti cha kuzaliwa au kama una namba ya NIDA.

“Na hapa nataka wananchi waelewe kuwa si kwamba hawatohesabiwa wasipokuwa na hivyo vitambulisho, lengo ni kutaka kujua idadi ya wananchi wenye vitambulisho vya taifa ili tunapoishauri serikali tuseme ni asilimia ngapi wana vitambulisho.

Na katika hili naomba pia ikiwezekana waviandae kabisa, ili karani akifika wanamwonyesha tu na si kwenda kutafuta maana inaweza kupoteza muda,” alisisitiza.

IFAHAMU maana ya Sensa ya watu na makazi 2022

IFAHAMU maana ya Sensa ya watu na makazi 2022KWA mujibu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) Sensa ya Watu na Makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum.

Kwa maana nyingine, sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi na hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi.

Takwimu hizi za msingi ndiyo zinazoweza kuanisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwemo makundi maalum yenye uhitaji maalum kwa mfano, watu wenye ulemavu, wanawake, watoto, vijana na wazee hivyo kurahisisha uandaaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji na mazingira yaliyopo.

Sensa ni zoezi la kuhesabu watu wote waliomo nchini, kujua mgawanyiko wa watu hao katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maeneo ya utawala na ukusanyaji wa taarifa nyingine zinazohusiana na watu na makazi yao.

HISTORIA YA SENSA TANZANIA.
Sensa ya kwanza Tanzania ilifanyika mwaka 1910. Sensa nne za Mwisho zilifanyika baada ya Uhuru, katika miaka ya 1967, 1978, 1988 na 2002.

Kulingana na SENSA ya mwisho iliyofanyika mwezi August 2002, idadi ya watu nchini Tanzania ilikuwa 34,443,603. Sensa ya 2012 itakuwa Sensa ya tano baada ya uhuru.

LENGO KUU LA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2012.
Kwa ujumla, takwimu za sensa ya watu ni za muhimu sana katika kupanga mipango inayohusiana na uchumi, utawala na huduma mbalimbali zinazohitajika katika kuinua hali ya maisha ya watu kitaifa.

Takwimu zitokanazo na Sensa uchangia katika uboreshaji wa maisha ya Watanzania kwa kutoa Takwimu sahihi na zinazoendana na wakati kwa ajili ya kutunga sera, kupanga mipango ya maendeleo na kuboresha utoaji wa huduma za jamii, ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa program mbalimbali zinazohusiana na maendeleo ya watu.

Sensa zote ni muhimu lakini Sensa ya mwaka 2022 ina umuhimu wake wa kipekee kwa kuwa itatoa viashiria vingi vitakavyotumika katika kutathimini program za MKUKUTA, MKUZA, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kwa Tanzania Bara na 2020 kwa Tanzania Zanzibar, Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano wa 2011/12-2015/16 na Malengo ya Milenia ifikapo 2025.

Viashiria hivi muhimu ni pamoja na idadi ya watu ki makazi, ukubwa wa nguvu kazi, idadi ya vifo na vifo vinavyotokana na uzazi, wastani wa umri wa kuishi wa Mtanzania, viwango vya uzazi, idadi ya watu wanaojua kusoma na kuandika na idadi ya watoto walioandikishwa shule.

Viashiria vingine ni pamoja na idadi ya kaya zinazoshujishughulusha na kilimo, ufugaji na uvuvi.

Madhumuni ya jumla ya kufanya sensa yamegawanyika katika sehemu kuu mbili;
Sehemu ya kwanza ni ya-kitakwimu na ya pili ni ya-kiutendaji.

2.Madhumuni ya kitakwimu:
Kupima hali ilivyo.
Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 itatoa takwimu kuhusu hali ya uchumi na ustawi wa jamii, kwa kuangalia mabadiliko yatakayoonekana kwenye sensa hiyo yakilinganishwa na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002, kama vile ongezeko na mgawanyiko wa watu ki-umri, ki-jinsi n.k.

2.1.Kutayarisha mipango ya Maendeleo
Inaeleweka kwamba, Sensa ya Watu hutoa takwimu zinazowezesha kupima kiwango cha maendeleo kilichofikiwa ili kuandaa sera na mipango ya maendeleo ya kipindi kinachofuata. Kwa hiyo, sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 itatoa, pamoja na mambo mengine, takwimu zitakazotumika katika kupima kiwango cha maendeleo kilichofikiwa na kupanga mipango ya maendeleo kwa wakati ujao.

2.3.Kuweka misingi itakayosaidia kufanya maamuzi
Idara za serikali na taasisi zake, mashirika yasiyo ya kiserikali, wafanya biashara, watafiti na watu binafsi, hutumia takwimu za sensa kama msingi wa kuboresha na kupanua shughuli zao.

2.4.Kupata takwimu kwa maeneo madogo madogo
Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, itawezesha upatikanaji wa takwimu muhimu kwa maeneo ya vijijini na mijini. Pia, wilaya zitapata takwimu za watu kuhusu hali zao za kiuchumi na ustawi wa jamii kwa ajili ya kutayarishia mipango yao ya maendeleo.

2.5.Kutoa mwongozo na msingi wa kufanya utafiti
Matokeo ya sensa, yatatoa takwimu muhimu ambazo zitatumika katika uchambuzi wa mabadiliko yaliyopo kuhusu mgawanyiko wa watu ki-umri, mtawanyiko na ongezeko la watu nchini. Hii itawezesha kuainisha maeneo ambayo yatahitaji kufanyiwa utafiti wa kina ili kuweza kujua chanzo cha hali iliyopo.

3.Madhumuni ya Kiutendaji:
Uundaji wa sampuli

Kuweka msingi imara wa sampuli utakaowezesha kuendesha tafiti mbalimbali kati ya sensa moja na nyingine pamoja na mipango mingine ya ki-Takwimu. Matokeo ya sensa yatasaidia kutoa takwimu za msingi zitakazosaidia katika kutayarisha msingi wa sampuli utakaotumika kufanyia tafiti zilizo bora kuhusu mambo ambayo yanatakiwa kutathminiwa mara kwa mara.

3.1 Kuweka msingi wa kuendesha sensa hapo baadae

Tanzania imeshafanya sensa nne baada ya kupata uhuru. Sensa hizi nne na ya mwaka 2012 zitatumika katika kuandaa na kuboresha sensa za baadaye.

Matumizi ya Takwimu zitokanazo na Sensa:
Utekelezaji wa shughuli hii ya kuhesabu watu kitaifa ni jambo la muhimu sana kwa Taifa. Matokeo ya sensa ya watu, yatatuwezesha kupata picha kamili juu ya watu waliomo nchini. Kwa maana hiyo, matokeo hayo yatakuwa ni msingi wa kupanga mipango ya maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii kama vile elimu, afya n.k

Mifano michache kuhusiana na suala hili na jinsi Takwimu za Sensa zinavyotumika kutekeleza mambo muhimu ya kisera ni kama hii ifuatayo:

Kwa mfano, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ingependa kupanua huduma za Afya ya Mama na Mtoto pamoja na kuwaelimisha watu kuhusu utunzaji wa mazingira katika maeneo ambamo matokeo ya sensa yanaonyesha viwango vya juu vya vifo.

.Takwimu kuhusu umri, zitaonyesha uwiano kati ya watoto ambao hawajafikia umri wa kwenda kuandikishwa/kuanza shule na wale ambao wamefikia umri huo; watu wanaojishughulisha na kazi za uzalishaji mali na wale wanaotoa huduma; vikongwe na wasiojiweza ambao wanahitaji msaada kutoka serikalini na wadau wengine ili waweze kuishi n.k.

Takwimu hizi vile vile, ni muhimu katika kupanga huduma za akina mama na watoto, shule na walimu, kuboresha huduma za afya, mazingira ya sehemu za kazi pamoja na kutafuta mbinu na kuweka mikakati ya kuinua maisha ya watu kwa ujumla.

Takwimu za elimu, darasa ambalo mtu anasoma au alilohitimu, zitaonyesha uwiano wa wanaojua kusoma na wasiojua kusoma, wenye viwango mbalimbali vya elimu, watoto wanaosoma shule ukilinganishwa na wale ambao walipaswa kuwa shuleni kutokana na umri wao n.k. Takwimu hizi zitakuwa ni kigezo muhimu katika kupanga mipango ya elimu ili kuimarisha juhudi za kuondoa umaskini, ujinga na maradhi.

Takwimu mbalimbali za kiuchumi, zitatuonyesha uwiano wa watu wanaojishughulisha na kazi za kuzalisha mali pamoja na aina ya kazi zinazofanywa na watu waliomo nchini. Hii itasaidia katika kupanga mipango ya maendeleo inayolenga katika kukuza ujuzi wa wafanyakazi, utoaji wa ajira kwa vijana, uboreshaji wa uzalishaji mali, na upangaji wa maisha bora zaidi kwa watu wote.
Takwimu kuhusu idadi ya watoto waliozaliwa hai na ambao bado wanaishi, na wale waliofariki, zitaonyesha hali ya uzazi na vifo hapa nchini.

Takwimu hizi, zitaonyesha jinsi watu wanavyoongezeka na kutuwezesha kufanya makisio ya idadi ya watu katika miaka ijayo kwa nchi nzima, ki-mkoa na ki-wilaya. Hii itatuwezesha kupanga mipango ya maendeleo kwa usahihi.

Takwimu za sensa zinasaidia katika kutathmini huduma za afya kwa watoto na kina mama. Hii ni muhimu katika kuweka mikakati ya kupambana na vifo vya watoto na vile vinavyosababishwa na matatizo ya uzazi kwa akina mama.

YAFUATAYO NI MAELEZO YA UFAFANUZI WA MALENGO YA MILLENIA, MKUKUTA, MKUZA NA DIRA YA MAENDELEO KATIKA KUHAMASISHA WADAU WA MAKUNDI YA JAMII.

LENGO
Kwa kuwa Takwimu za Sensa Zitatumika kutathmini malengo ya millennia, ni budi kutoa ufafanuzi na maana na kuwapa elimu wadau wa Sensa kuhusiana na malengo ya millennia, Mkakati wa Kupunguza Umasikini na kukuza Uchumi (MKUKUTA) na MKUZA kwa Tanzania visiwani pamoja na Dira ya Maendeleo

1. MALENGO YA MILLENIA
Malengo ya Millenia kama inavyoitwa kwa kiingereza Millenium Development Goals (MDGs) yalipangwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2000 kule Marekani. Malengo yanatekelezwa kati ya 2000 2015. Malengo haya yako nane nayo ni;
1.1. Kuondoa Umasikini uliokithiri
1.2. Kufikia Elimu ya Msingi kwa Wote
1.3. Usawa wa Kijinsia na kuwawezesha wanawake
1.4. Kupunguza Vifo vya watoto
1.5. Kuboresha Afya ya akina mama wazazi
1.6. Kupambana na Ukimwi na Virusi vya Ukimwi na Kinga
1.7. Kuhakikisha mazingira endelevu
1.8. Kuendeleza Mshikamano wa Kimataifa kwa maendeleo

2. MKUKUTA
MKUKUTA ni neno maarufu katika jamii ya Tanzania toka ulipozinduliwa mwaka 2005.

Kirefu chake kikiwa ni Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania. Hivi sasa tuna Mkukuta II ambao umeboreshwa kutoka katika Mkakati wa kwanza wa kupunguza umaskini uliozinduliwa Oktoba 2000 na kutekelezwa kuanzia 2005 hadi 2010
Malengo ya Mkukuta yamejikita katika;

· Ukuaji wa Uchumi
· Kupunguza Umasikini wa Kipato

3. MKUZA
Malengo ya MKUZA ni;
-Kupunguza Umasikini wa kipato
-Kuweka mazingira mazuri kwa uwekezaji

4.DIRA YA MAENDELEO
Malengo makuu yamegawanyika katika nguzo nne ambazo ni;
4.1. Nguzo ya kwanza ni kuendeleza Utulivu wa amani

4.2.Nguzo ya pili ni kutumia fursa na rasilimali tele za Tanzania (Watu takribani milioni 40, ardhi nzuri ya kutosha, madini ya kila aina, bahari, maziwa, mito, misitu, wanyama pori, mifugo, vivutio vya Utalii kemkem n.k) kama mota ya kukuza uchumi

4.3. Nguzo ya tatu ni kutumia nafasi nzuri sana ya Tanzania kijiografia. Lengo ni kuifanya nchi hii kuwa lango kuu la biashara na kuhudumia nchi za maziwa makuu na hasa zile zisizokuwa na mlango bahari (DRC Mashariki, Rwanda, Burundi, Uganda, Zambia, Malawi).

Kipaumbele ni kukarabati/kujenga kwanza miundombinu ya kimkakati hasa nishati, bandari, reli, barabara teule na mkongo wa taifa ili kuiwezesha Tanzania kuwa na uchumi shindani pamoja na kuongeza ufanisi katika huduma hizo na zile za Mamlaka ya Mapato.

4.4. Nguzo ya nne ni kukuza matumizi ya TEHAMA (ICT) kama nyenzo ya kuongeza tija hasa kilimo cha mazao, ufugaji na uvuvi na pia viwanda vinavyotumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.