Matokeo Benin vs Tanzania + Msimamo

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Benin kwenye mchezo wa kufuzu Fainali za kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.
Mchezo huo ulichezwa kwenye dimba la Stade de I’amitie Mathieu Cotonou nchini Benin leo Jumapili October 10,2021 kuanzia majira ya saa 10:00 jioni.
Goli pekee na la ushindi la Tanzania limekwamishwa wavuni katika kipindi cha kwanza na Mshambuliaji Simon Msuva kwenye dakika ya 6’ kwa mkwaju mkali uliomshinda mlinda mlango wa Benin.
Kwa matokeo hayo sasa Tanzania inaongoza kundi J kwa kufikisha alama 7 sawa na Benin wakitofautiana magoli ya kufunga na kufungwa.
Tanzania imebakiza mechi mbili tu kukamilisha mzungo wa kundi J dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC itakayochezwa Jijini Dar, na mechi ya mwisho dhidi ya Madagascar ugenini.
Msimamo wa Kundi J, Kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar baada ya michezo minne kwa kila timu.
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: Benin vs Tanzania, Matokeo Benin vs Tanzania, Msimamo kundi J, Tanzania vs Benin