Nijuze Habari

Matokeo KMC FC vs Simba SC

Filed in Michezo by on 24/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

MABINGWA watetezi, Simba SC imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1vdhidi ya KMC FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) Uwanja wa Alli Hassan Mwinyi Mjini Tabora.

Mabao ya Simba SC yamefungwa na mabeki, Mohamed Hussein ‘ Tshabalala’, dakika ya 10, Joash Onyango dakika ya 12 na mshambuliaji Kibu Dennis akifunga mawili dakika ya huku KMC limefungwa na Abdul Hillary dakika ya 39.

Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 21, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na vinara, Young Africans SC baada ya timu zote kucheza mechi tisa.

KMC yenyewe inabaki na pointi zake 10 katika nafasi ya 11 baada ya kucheza mechi 10 sasa.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, wenyeji, Coastal Union wameibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 10 na la penalti dakika ya 90 na lingine Hajji Ugando dakika ya 45, wakati ya Mbeya City yakifungwa na Juma Luizio dakika ya 33 na Richardson Ng’ondya kwa penalti dakika ya 72.

Coastal Union inafikisha pointi 17 na kupanda nafasi ya tatu ikiizidi pointi mbili Mbeya City inayoshukia nafasi ya sita baada ya timu zote kucheza mechi 10 sasa.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.