Nijuze Habari

Matokeo KMKM FC vs Yanga SC November 12,2021

Filed in Michezo by on 12/11/2021 0 Comments

KLABU ya Young Africans SC imekamilisha michezo yake ya kirafiki visiwani Zanzibar kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMKM FC, mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Amaan visiwani humo leo Ijumaa November 12,2021.

Nijuze Habari Application

KLABU ya Young Africans SC imekamilisha michezo yake ya kirafiki visiwani Zanzibar kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMKM FC, mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Amaan visiwani humo leo Ijumaa November 12,2021.

Soma: Magazeti ya Ijumaa November 12,2021

Mabao ya washambuliaji Wakongomani Jesus Moloko na Fiston Kalala Mayele yametosha kuipa ushindi Klabu hiyo, huku ikitanguliwa kufungwa bao na KMKM FC kwenye kipindi cha kwanza.

Soma: Tanzania yatupwa nje kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar 2022

Klabu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Jangwani Jijini Dar es salaam ilicheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki visiwani humo Jumanne hii na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mlandege, ushindi wa leo unafanya idadi ya michezo iliyocheza bila kufungwa kufika takribani 10.

Baada ya kukamilika kwa michezo Klabu hiyo sasa inarejea Jijini Dar es salaam kukamilisha maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi ya November 20,2021 kwenye uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

Soma: Matokeo ya Darasa la Saba 2021

telegram Nijuze Habari

Tags: , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.