Nijuze Habari

MATOKEO Ligi Kuu Tanzania Bara June 13,2022

Filed in Michezo by on 13/06/2022 0 Comments

MATOKEO Ligi Kuu Tanzania Bara June 13,2022WENYEJI, Geita Gold wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC, mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita.

Nijuze Habari Application

MATOKEO Ligi Kuu Tanzania Bara June 13,2022

MATOKEO Ligi Kuu Tanzania Bara June 13,2022WENYEJI, Geita Gold wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC, mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita.

Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Edmund John dakika ya 45 na George Mpole dakika ya 78 na kwa ushindi huo Geita wanafikisha pointi 39 baada ya kucheza michezo 27.

Ushindi huo umeifanya Geita Gold Kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye Msimamo wa Ligi ikiizidi pointi 2 Namungo FC ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi.

Dodoma Jiji baada ya kichapo cha leo ukiwa ni mchezo wa 27 inabaki na pointi zake 31 na kushuka kwa nafasi moja hadi ya 12 kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League 2021/2022).

MATOKEO Ligi Kuu Tanzania Bara June 13,2022Katika mchezo uliotangulia mchana, wenyeji wengine, Mtibwa Sugar waliichapa Ruvu Shooting mabao 3-1, mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Ally Kombo aliyejifunga dakika ya 41 na Brian Mayanja mawili, dakika ya 56 na 76, wakati la Ruvu Shooting likifungwa na Abal Kassim dakika ya 86.

Ushindi huo unaifanya Mtibwa Sugar kufikisha pointi 31 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 11, wakati Ruvu Shooting ikibaki na pointi zake 28 kwenye nafasi ya 13 baada ya timu zote kucheza michezo 27.

UNAWEZA PIA KUSOMA👇👇👇

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.