Nijuze Habari

Matokeo Mlandege FC vs Yanga SC

Filed in Michezo by on 09/11/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

KLABU ya Young Africans SC imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake baada ya kuichapa Mlandege FC bao 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar.

Kipindi cha Kwanza kiliisha kwa sare ya bila kufungana, ambapo Yanga ilirejea ikiwa imara zaidi katika kipindi cha pili na kufanikiwa kupata bao pekee la ushindi kwenye dakika ya 49 kupitia kwa mshambuliaji Heritier Ebenezer Makambo.

Makambo alifanikiwa kufunga bao hilo akimalizia mpira uliopigwa na Mshambuliaji Mkongomani mwenzake Fiston Kalala Mayele ambao uligonga mwamba kabla ya kuukutana.

Aidha Klabu hiyo inaendelea kusalia visiwani Zanzibar ambapo Ijumaa hii ya November 12 watashuka tena uwanja wa Amaan kuikabili KMKM ya Visiwani humo ukiwa ni mchezo wa Kirafiki pia.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.