Nijuze Habari

Matokeo + Msimamo NBC Premier League October 22,2021

Filed in Michezo by on 22/10/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

BAO pekee la mshambuliaji Dickson Mhilu dakika ya 38 limetosha kuwa Kagera Sugar FC ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar FC jioni ya leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba mkoani Kagera.

Ushindi huo wa kwanza katika michezo minne ya mwanzo, kufuatia kufungwa 1-0 na Young Africans SC nyumbani na sare mbili mfululizo ya 1-1 dhidi ya Namungo FC mjini Lindi na ya 0-0 dhidi ya Mbeya City FC hapo hapo Kaitaba unaifanya Kagera Sugar ifikishe pointi tano.

Hali ni mbaya kwa Mtibwa Sugar baada ya kucheza mechi nne bila ushindi, kufuatia kufungwa bao 1-0 na Mbeya Kwanza Mlandizi na sare mbili ya 0-0 dhidi ya Tanzania Prisons Jijini Dar es Salaam na ya 1-1 na Geita Gold Mjini Geita.

Baada ya mchezo huo huu ni Msimamo wa Ligi Kuu hiyo ya NBC.

Dickson Mhilu akikabidhiwa Zawadi ya Mchezaji Bora wa Mchezo huo.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.