Matokeo Namungo FC vs Yanga SC November 20,2021
JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA
JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA
AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Klabu Young Africans SC imepunguzwa kasi katika Ligi Kuu hiyo baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji, Namungo FC kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi.
Namungo FC walitangulia kwa bao la mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa akiifunga timu yake ya zamani dakika ya 52, kabla ya kiungo Saido Ntibanzokiza kuifungia Young Africans bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati dakika ya 81.
Baada ya sare hiyo Young Africans inafikisha pointi 16 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa pointi mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC baada ya timu zote kucheza mechi sita.
Michezo mingine Ligi Kuu leo, Geita Gold wakiwa ugenini wamefanikiwa kuibuka na ushindi mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar FC kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mabao ya Geita Gold yamefungwa na George Mpole yote mawili dakika ya pili ya mchezo na ya 35, huku bao pekee la Kagera Sugar likifungwa na Mbaraka Yussuf kwenye dakika ya 10.
MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.
Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.
Baada ya ushindi huo Geita inafikisha pointi tano na kujiinua kidogo kutoka nafasi ya 15 hadi ya 13 kwenye Msimamo wa Ligi, huku wakati Kagera Sugar ikibaki na pointi zake nane katika nafasi ya sita baada ya timu zote kucheza mechi sita.
Mchezo wa mapema leo Mbeya City imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Juma Luizio dakika ya 45, Juma Shemvuni dakika ya 60 na Suleiman Ibrahim dakika ya 85, wakati la Mtibwa limefungwa na Salum Kihimbwa dakika ya 82 kwa mkwaju wa penati.
Kwa ushindi huo, Mbeya City inafikisha pointi 10 na kupanda hadi nafasi ya tatu ikiizidi wastani wa mabao tu Polisi Tanzania baada ya wote kucheza mechi sita
Mtibwa yenyewe inabaki na pointi zake mbili baada ya mechi sita kwenye katika nafasi ya 14 kwenye, ikizizidi wastani wa mabao tu Geita Gold na KMC zilizo chini yake mkiani kwenye eneo la kushuka moja kwa moja.
Ikumbukwe timu zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Tags: Matokeo Namungo FC vs Yanga SC, Matokeo NBC Premier League, Yanga SC vs Namungo FC