Nijuze Habari

Matokeo NBC Premier League December 05,2021

Filed in Michezo by on 05/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

KLABU ya KMC FC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold Katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Mabao ya KMC yamefungwa na Abdulrazak Hamza dakika ya 47 na Matheo Anthony dakika ya 59.

Kwa ushindi huo, KMC imefikisha pointi tisa na kusogea hadi nafasi ya nane, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake tano katika nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16, baada ya wote kucheza mechi nane.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu, wenyeji, Coastal Union wameichapa timu nyingine iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, Mbeya Kwanza mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanya.

Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Vincent Abubakar dakika ya pili na Amani Kyata dakika ya 76, wakati la Mbeya Kwanza limefungwa na Willy Edgar dakika ya 48.
Coastal Union inatimiza pointi 11 na kupanda hadi nafasi ya sita, wakati Mbeya Kwan inabaki na pointi zake saba katika nafasi ya 13 baada ya timu zote kucheza mechi nane.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.