Nijuze Habari

MATOKEO NBC Premier League June 29,2022

Filed in Michezo by on 29/06/2022 0 Comments

MATOKEO | Funga dimba ya msimu #NBCPL2021_22

Nijuze Habari Application

MATOKEO NBC Premier League June 29,2022, Funga dimba ya msimu.

MATOKEO | Funga dimba ya msimu #NBCPL2021_22

FT Kagera Sugar FC 0-0 Polisi Tanzania FC
FT Mbeya Kwanza FC 0-0 Simba SC
FT Young Africans SC 1-0 Mtibwa Sugar FC
FT Dodoma Jiji FC 1-0 KMC FC
FT Ruvu Shooting FC 1-0 Tanzania Prisons FC
FT Coastal Union FC 1-1 Geita Gold FC
FT Mbeya City FC 1-1 Namungo FC
FT Azam FC 4-1 Biashara United FC

MSIMAMO NBC Premier League June 29,2022MSIMAMO: Biashara United wanaungana na Mbeya Kwanza kushuka daraja, wakati mtibwa na Tanzania Prisons wakilazimika kwenda kwenye mtoano (Play-Off) ili kujitetea.

Rasmi, Mbeya Kwanza FC ya Mkoani Mbeya na Biashara United FC ya Mkoani Mara zimeshuka daraja moja kwa moja, Mtibwa Sugar FC ya Morogoro na Tanzania Prisons FC ya Mbeya wao watacheza Play Off kupambania kubaki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao wa 2022/2023 na timu aombaye itaenda kucheza Play Off na JKT Tanzania FC.

George Amani Mpole Geita Gold FCRasmi, Mshambuliaji wa Geita Gold FC ya Mkoani Geita, George Enock Mpole ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League 2021/2022) akiwa na mabao 17 mbele ya Mshambuliaji wa Young Africans SC, Fiston Kalala Mayele aliyemaliza na mabao 16.

Yanga SC Bingwa NBC Premier League 2021/2022Rasmi Young Africans SC wanaweka rekodi ya kumaliza msimu huu wa 2021/2022 bila kupoteza mchezo hata mmoja, rekodi kama hii iliwekwa na Simba SC msimu wa 2009/2010 wakimaliza msimu bila kupoteza na msimu wa 2013/2014 Azam FC wakimaliza msimu bila kupoteza.

Vilabu vya Young Africans SC na Simba SC vitashiriki Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika (CAF Champions League) Kwa msimu wa 2022/2023, Azam FC wao watashiriki Kombe la Shirikisho (CAF Confederations Cup) na wataungana na Coastal Union au Geita Gold FC kushiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Coastal Union wanaweza kushiriki Mashindano hayo endapo watakuwa washindi wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la TFF maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) mbele ya Young Africans SC, mchezo wa Fainali unaotajiwa kupigwa July 02,2022.

VINARA WA MABAO: Hawa ndiyo waliomaliza msimu wakiwa na angalau mabao matano kwenye ligi kuu.VINARA wa Ufungaji NBC Premier League 2021/2022

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.